Kundi la wasanii wa uchoraji la 14+ ikiwa katika maonyesho ya uchoraji picha katika maeneo ya wazi.
Msemaji
wa kundi la 14 +, Aman Abeid akitoa maelezo kwa afisa habari wa Barza
la Sanaa nchini (BASATA) Agnes Kimwaga wakati wa maonyesho hayo
Mchoraji
Nguli wa sanaa za uchoraji, Raza Muhamed akichora wakati wa maonyesho
hayo ya uchoraji wa moja kwa moja katika eneo la wazi
Mchoraji
Lutengano Mwakisopile akionyesha ufundi wake wa kuchora katika eneo la
busatani ya kaburi moja Posta jijini Dar es Salaam
Mchoraji Chilonga Haji akionyesha umahiri wake wa kuchora katika maonyesho hayo
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Baraza
la Sanaa nchini (BASATA) limeziomba tasisi za Serikali na mashirika
mbalimbali kuweza kununua kazi za Sanaa za uchoraji za wasanii
watanzania na kuacha kununua michoro kutoka nje ambayo aina ubora.
Hayo
yamesemwa na Afisa habari wa Basata, Agnes Kimwaga alipotembelea
maonyesho ya wazi ya uchoraji wa michoro mbalimbali yaliyoandaliwa na
kundi la 14 + la hapa nchini.
“Sanaa
za uchoraji na uchongaji za hapa nchini zinatengenezwa katika ubora wa
hali ya juu ndio maana michoro mingi inayopelekwa nje kutoka hapa
inapata sifa kubwa hivyo ni wakati wa tasisi zetu za umma na ofisi za
serikali kuanza kupambwa na michoro hii” amesema Agnes.
Kwa
upande wake kiongozi wa kikundi cha 14 +, Lutengano Mwakisopile
amewataka watanzania kuendelea kuwaonga mkono katika harakati zao hili
waweze kujivunia sanaa hiyo kama ilivyo kwa nchi jirani.
Mchoraji Mins Mims akionyesha ufundi wake wa kuchora katika maonyesho hayo
Mchoraji Caludia Chatanda akitoa maelezo kwa watu waliofika katika maonyesho hayo
Mchoraji wa vibonzo Nathan Mpangala akichora mchoro wake mbele ya wadau katika maonyesho hayo ya wazi
Nathan Mpangala akitoa somo kwa wadau wakifika katika maonyesho hayo
Mchoraji kutoka Vipaji House akionyesha umahiri wake wa kuchora katika maonyesho hayo
wanafunzi wakitazama kwa makini moja ya michoro iliyochorwa na wasanii wa kundi la 14+
SHARE
No comments:
Post a Comment