MBUNGE
wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi
(CCM) akimkabidhi mifuko ya saruji kwa ajiri ya ujenzi wa jengo la
ofisi ya chama katika kata ya Ruaha kwa mwenyekiti wa chama cha
mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa Abeid Kiponza
MBUNGE
wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi
(CCM) akiwa katika eneo la uwanja wa kujenga ofisi ya kata ya Ruaha
MBUNGE
wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi
(CCM) akibadilishana mawazo na katibu wa ccm manispaa ya Iringa Nuru
Ngereja
MBUNGE
wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi
(CCM) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa hama hicho
wa kata ya ruaha
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa Abeid Kiponza pamoja na viongozi wengine wa chama hicho.
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati akipokelewa na wanachama wa mtaa wa kigamboni mkoani Iringa
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MBUNGE
wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi
(CCM) ameanza kusaidia Ujenzi wa ofisi za Matawi ya CCM katika kata
mbali mbali za Jimbo la Iringa mjini kama sehemu ya majukumu yake ya
kukijenga chama hicho ambacho kilipoteza kiti cha ubunge na halmashauri
kuchukuliwa na wapinzani.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi mifuko ya saruji kwa Ujenzi wa ofisi za Tawi
Kigamboni na Ruaha ,Kabati alisema kuwa anafanya hivyo kama njia ya
kutekeleza ilani na maadhimio ya miaka arobaini ya chama cha mapinduzi.
“Nakipenda
chama changu ndio maana napigana sana kuhakikisha chama cha mapinduzi
mkaoni mhapa iringa kinarudi mahala pake na kuhakikisha kinaaminika kwa
wananchi na wanachama wa manispaa ya Iringa”.alisema Kabati
Hata
hivyo Kabati alisema kuwa ataendelea kusaidia Ujenzi wa ofisi hizo ili
kuona ndani ya kipindi kifupi cha miezi mitatu ama sita kila tawi
linakuwa na ofisi yake ya tawi na aliwataka wanachama wa CCM kushikamana
na kuendelea na Ujenzi wa ofisi hizo pamoja na kujihusisha na shughuli
nyingine za kijamii
"Haiwezakani
chama kikubwa kama hiki kukosa ofisi za matawi wakati tunamaeneo mengi
ya kujenga ofisi nitakikisha tunashirikiana na wanachama na wananchi
wengine kujenga hizo ofisi ili kumuunga mkono Rais wetu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania DR John Pombe Magufuli ambaye anapambana
kuhakikisha cha mapinduzi kinakuwa chama cha wananchi wa chini na sio
matajiri pekee yao".alisema Kabati
Kwa
upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa
Abeid Kiponza aliwataka wanachama kuwa kusahau yaliyopita na kuanza
kujenga chama upya.
“Tulipoteza
halmashauri ya Iringa na jimbo hivyo inabidi tukae chini na tujipange
upya kukijenga chama maana tunajua kwa kujenga ofisi za matawi
zitatusaidia kurudisha hadhi na hali ya chama hapa manispaa kwa kutoa
huduma bora kwa wananchi wote bila kuchagua chama”.alisema Kiponza
Kiponza
alimshukuru mbunge wa viti maalumu Ritta kabati kwa mchango anaoutoa
kwa kuleta maendeleo katika manispaa ya Iringa hasa ukiangalia ujenzi wa
majengo mbalimbali ya shule,taasisi za kidini,taasisi za kijamii hapa
kujenga majengo ya chama.
Lakini Kiponza alimtaka mbunge Kabati kuwasaidia wananchi wanaodhurumiwa na kunyang’anywa mali zao katika manispaa ya Iringa.
“Hapa
kigamboni kunawananchi wanapigwa na viongozi wa mtaa kwa kuwa wapo CCM
tu na wamenyang’anywa kituo cha kuchotea maji ambacho kilikuwa mradi wa
chama cha mapinduzi hivyo lazima upambane kuhakikisha wananchi wanaishi
kwa amani na mali za chama zinarudi kwenye chama”.alisema Kiponza
Naye
Katibu wa CCM manispaa ya Iringa Nuru Ngeleja alisema kuwa wamejipanga
kuhakikisha ofisi zote za chama zinajengwa na zinakuwa katika ubora
unaotakiwa kutokana na ukubwa wa chama cha mapinduzi(CCM) na kuahidi
kuwa wataendelea kumuunga mkoano Rais wa jamhuri ya muungano ya Tanzania
Dr John Pombe Magufuri.
“Sisi
tunafanyakazi ya kumsaidia mwenyekiti wetu wa chama ambaye ni Rais wetu
kwa kufanya kazi na kuisimamia serikali kufanya kazi kwa uhakika na
kuwafaikia na kuwatumikia wananchi waliowaweka madarakani mpaka sasa”.
Alisema Ngereja
SHARE
No comments:
Post a Comment