AWAPA SIKU 14, WAFANYA BIASHARA NJE YA SOKO KUAMIA NDANI YA SOKO
Na Anthony John Glob Jamii.
MKUU
wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ameendelea na ziara ya kutembelea Kata
za wilaya ya kinondoni, ikiwa siku ya pili ya ziara yake mkuu wa wilaya
ametembelea kata Mzimuni, akiwa katika soko la Magomeni, ametoa siku 14
kwa uongozi wa soko hilo kuhakikisha wanaondoa baa na ghala vilivyopo
katikati ya soko hilo.
Akiwa ndani ya soko hilo, Hapi alisema inasikitisha kuona hata wamiliki wa ghala hizo hawafahamiki.Alisema uwepo wa ghala na baa katikati ya soko hilo inasababisha kuwanyima fursa wafanyabiashara walio wengi hasa wale wadogo.
"Ninatoa
siku 14 kwa viongozi wa soko na manispaa kuhakikisha wanaaondoa maghala
haya kwani inaonyesha ni ya wafanyabiashara wakubwa hivyo waende kwa
wenzao hapa hapawafai,"alisema Hapi.
Sambamba
na hilo mkuu huyo ametoa siku 14 nyingine kwa wafanyabiashara
wanaofanya biashara nje ya soko hilo kurejea ndani ya.soko.Alisema sheria zipo wazi na hakuna aliyejuu ya sheria zaidi ya kuzingatia sheria hizo.
"Hakuna
aliyeruhusu wafanyabiashara wengine kufanya biashara nje ya soko,
hivyo naagiza ndani ya siku 14 wote mhamie ndani kwa sababu mnaleta
usumbufu kwa wengine na kuleta malalamiko,"alisema Hapi.
Baadae
mkuu wa wilaya alifanya mkutano wa adhara katika shule msingi Mikumi,
katika mkutano huo wananchi waliuliz maswali mbali mbali lakini kero
kubwa imeonekana kuwa viongozi wao sio waaminifu hukusanya pesa kwa
wananchi lakini hafanyi yaliyokusudiwa, mkuu wa wilaya akijibu hoja hiyo
ameagiza viongozi wote kutoa risit za EFD kwa kila malipo yanapofanyika
SHARE
No comments:
Post a Comment