Rais
Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete jana tarehe 20 Februari 2016 amekutana na kufanya
mazungumzo na Rais wa Chad, Mhe. Jenerali Idrissa Deby Itno katika
Ikulu yake jijini N'Djamena, Chad. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na
Waziri wa Elimu wa Chad Mhe. Ahmat Ghazali Acyl na Waziri wa Fedha Mhe.
Diguimbaye Christian.
Ziara
hiyo ya Rais Mstaafu nchini Chad ni muendelezo wa Kamisheni ya
Kimataifa ya Elimu ya kuwafikia viongozi wa nchi 14 za Afrika za
kipaumbele katika kutekeleza mapendekezo ya Ripoti ya Kizazi cha Elimu
(The Learning Generation).
Katika
mazungumzo yao, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji
wake Rais Deby wamezungumzia janga kubwa linaloinyemelea dunia na hasa
nchi za uchumi wa kati na chini ikiwa hakutafanyika mapinduzi makubwa
katika sekta ya elimu.
Viongozi
hao wamezungumzia haja ya nchi za bara la Afrika kuchukua hatua z
amakusudi kufanya maboresho na mageuzi makubwa katika sekta ya elimu
katika nchi zao ili kuweza kuendana na kasi ya nchi zilizoendelea. Azma
hiyo inatokana na stadi kuwa nchi za uchumi wa kati na chini zko nyuma
kielimu kwa miaka 50 hadi 70. Aidha, lipo tishio kuwa ifikapo mwaka
2050, kazi na ajira takribani bilioni 2 zitakuwa zimefutwa kutokana na
maendeleo na matumizi ya teknolojia (automation).
Rais Deby
amemuhakikishia Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete uthabiti wa
azma ya nchi yake kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu.
Ameelezea utayari wa nchi yake kujiunga na mpango huo wa kufanikisha
mapinduzi ya sekta ya elimu ndani ya kizazi kimoja ifikapo mwaka 2040.
Mbali
na mkutano wake na Rais wa Chad, Rais Mstaafu amekutana pia na kufanya
mazungumzo na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika na Aliyekuwa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad Mhe Moussa Fakhi nyumbani kwake
N'Djamena. Rais Mstaafu amempongeza Mhe. Fakhi kwa kuchaguliwa na Wakuu
wa Nchi wa Umoja wa Afrika kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja huo na
kumtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya. Viongozi hao wawili
wamekuwa pia na mazungumzo yaliyohusu mipango ya Kamisheni ya Kimataifa
ya Elimu barani Afrika na masuala ya hali ya usalama ya Libya.
Rais
Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Chad, Mhe. Jenerali Idrissa Deby
Itno katika Ikulu ya nchi hiyo jijini N'Djamena, Chad.
Rais
Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Chad, Mhe. Jenerali Idrissa Deby
Itno katika Ikulu ya nchi hiyo jijini N'Djamena, Chad.
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mwenyekiti
Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika na Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje
wa Chad Mhe Moussa Fakhi nyumbani kwake jijini N'Djamena
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika Mhe Moussa Fakhi nyumbani kwake jijini N'Djamena
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika Mhe Moussa Fakhi nyumbani kwake jijini N'Djamena.
SHARE
No comments:
Post a Comment