Ijumaa
Februari 24,2017 Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imezikutanisha
Asasi za Kiraia zilizopo katika manispaa hiyo kwenye semina ya siku moja
iliyolenga kuzijengea uwezo ili ziweze kutekeleza vyema shughuli zao
katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Mgeni
rasmi katika semina hiyo ya siku moja iliyofanyika katika ukumbi wa
Lewis Kalinjuna uliopo katika manispaa ya Shinyanga alikuwa Mkuu wa
wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.
Akizungumza
wakati wa kufungua semina hiyo Matiro amezitaka asasi za kiraia
(NGO’s,CBO’) kuepuka kuwa sehemu ya kushiriki uovu katika jamii
wakitumia mwamvuli wa asasi na kuzitaka kuepuka kuilaumu serikali badala
ya kuishauri pale inapokosea.
“Serikali
inatambua kazi nzuri zinazofanywa na asasi za kiraia katika kuisaidia
jamii,nyinyi ni sehemu ya serikali,mnafanya kazi pamoja na serikali
kuisaidia serikali,serikali yetu haiwezi kufanya kila kitu,hivyo
haipendezi kuilaumu serikali,ishaurini pale mnapoona mambo hayaendi
sawa”,amesema Matiro.
“Pia
msiwe na usiri katika shughuli zenu maana zipo asasi zinaingia kimya
kimya katika jamii,kabla ya kuanza kutekeleza mradi jitambulishe katika
jamii,elezeni mnafanya nini pia itatusaidia kujua asasi ipi inafanya
nini hali ambayo itawezesha kupungua kwa idadi ya asasi zinazofanya
shughuli moja katika eneo moja”, ameongeza Matiro.
Naye
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geoffrey Ramadhan Mwangulumbi
amesema asasi za kiraia zinatakiwa kuwajibika kwa serikali hivyo
zinatakiwa kuwa zinatoa taarifa serikalini kuhusu shughuli wanazofanya.
Miongoni
mwa mada zilizotolewa katika semina hiyo ni pamoja na sheria za
uendeshaji wa asasi za kiraia,taratibu za uendeshaji wa asasi za
kiraia,namna ya kuandaa andiko la mradi na masuala yanayohusu rushwa.
Mwenyekiti
wa semina hiyo Mchungaji Dkt. Meshack Kulwa kutoka TCCIA Shinyanga
akimkaribisha mgeni,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ili
afungua semina hiyo.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufungua
semina hiyo ambapo alisema serikali inatambua kazi nzuri zinazofanywa na
asasi za kiraia na ipo tayari kushirikiano na asasi yoyote katika
kuwaletea maendeleo wananchi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini.Kulia ni Naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo ukumbini
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na viongozi wa asasi za kiraia katika manispaa ya Shinyanga
Naibu
meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya akizungumza ukumbini.Kulia
ni Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Geoffrey Ramadhan Mwangulumbi
Mkurugenzi
wa manispaa ya Shinyanga Geoffrey Ramadhan Mwangulumbi akizungumza
katika semina hiyo ambayo imekutanisha viongozi mbalimbali wa asasi za
kiraia katika manispaa hiyo
Washiriki wa semina hiyo wakiwa ukumbini
Mkurugenzi
wa manispaa ya Shinyanga Geoffrey Ramadhan Mwangulumbi akisisitiza
asasi za kiraia kushirikiana na serikali katika kuiletea maendeleo jamii
Afisa
Uchunguzi Mwandamizi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) mkoa wa Shinyanga Alice Mazoko akitoa mada kuhusu masuala ya
rushwa ambapo alizitaka asasi hizo kujikita katika malengo yao badala ya
kugeuka kichochoro cha kuchuma pesa zisizokuwa halali (rushwa).
Afisa
Uchunguzi Mwandamizi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) mkoa wa Shinyanga Alice Mazoko akisisitiza juu ya umuhimu wa
asasi za kiraia kuepuka vitendo vya rushwa katika shughuli zao.
Lubumba
Masebu kutoka asasi ya vijana ya Youth Development Organisation (YUDEN)
akichangia hoja wakati wa semina hiyo ambapo alisema asasi nyingi
hazifanikiwi kutokana na jamii kukosa elimu na kushindwa kuelewa malengo
ya miradi husika
Mchumi wa manispaa ya Shinyanga,Alex Mpasa akitoa mada kuhusu namna ya kuandaa andiko la mradi
Mchumi
wa manispaa ya Shinyanga,Alex Mpasa akiendelea kutoa mada.Kulia ni
katibu wa chama cha watu wenye ualbino Lazaro Nael akimsaidia
mawasiliano kwa njia ya ishara mmoja wa washiriki mwenye ulemavu wa
kusikia (asiyesikia)
Mwezeshaji akitoa mada ukumbini
Washiriki wakiwa ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini….
Semina inaendelea
Washiriki wakiwa ukumbini
Semina inaendelea
Semina inaendelea
Viongozi wa asasi za kiraia wakiwa ukumbini
Mwezeshaji akitoa mada kuhusu sheria za uendeshaji wa asasi za kiraia
Afisa Maendeleo ya Jamii manispaa ya Shinyanga Salome Komba akitoa mada kuhusu taratibu za uendeshaji wa asasi za kiraia.
SHARE
No comments:
Post a Comment