TRA

TRA

Saturday, February 25, 2017

TIGO YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO KWA KITUO CHA AMANI MKOANI KILIMANJARO

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata akitoa maelezo ya msaada wa vifaa vya michezo mbalimbali pamoja na vifaa vya Kilimarathon, vifaa hivyo vimetolewa kwa Kituo cha watoto cha Amani Children’s Home cha mjini Moshi, Kilimanjaro, Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Meindert Schaap.
 
 Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata (kulia) akimkabidhi jezi Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha watoto cha Amani Children’s Home cha mjini Moshi, Kilimanjaro, Meindert Schaap ikiwa ni sehemu ya msaada wa vifaa vya michezo uliotolewa na Tigo kwa ajili ya kituo hicho.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha watoto cha Amani Children’s Home cha mjini Moshi, Kilimanjaro, Meindert Schaap akitoa shukrani kwa mtandao wa simu za mkononi wa Tigo baada ya kupokea msaada wa vifaa vya michezo mbalimbali vikiwemo vya Kilimarathon. Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata

Watoto cha Amani Children’s Home cha mjini Moshi, Kilimanjaro pamoja na  wafanyakazi wa Tigo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mtandao huo kukabidhi vifaa vya michezo.

Mtoto anayelelewa na  Amani Children’s Home cha mjini Moshi, Kilimanjaro, Joyce Nganda akitoa neno la shukrani kwa waandishi wa habari baada ya kituo hicho kupokea msaada wa vifaa vya michezo kutoka Tigo.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger