Rais wa Rwanda, Paul Kagame
Kiongozi wa
upinzani nchini Rwanda, ametangaza kuunda serikali sambamba na utawala
uliopo Rwanda, lakini itakayokuwa ikifanya kazi nje ya nchi.
Thomas
Nahimana ambaye ni kasisi wa zamani anayeishi nchini Ufaransa
ametangaza kuunda serikali hiyo itakayofanyia kazi uhamishoni. Katika mazungumzo na BBC, mwanasiasa huyo anasema lengo la serikali yake ni kuiondoa madarakani serikali ya rais Paul Kagame, anayemlaumu kuvunja sheria na kukandamiza wananchi.
Thomas Nahimana, amekatazwa kuingia Rwanda kujiandikisha kama mgombea wa kiti cha urais, katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.
Baraza lake la mawaziri
Ametangaza tayari baraza lake la mawaziri.- Rwanda kuwapeleleza askari 20 wa Ufaransa
- Rwanda yanunua ndege ya kisasa ya Airbus
- Kagame: Raia wa Rwanda walitaka wenyewe
Bw Nahimana, ambaye ni mhutu, amelaumiwa kwa kuandika taarifa kadhaa za kikabila na kumkosoa rais Paul Kagame.
Chama chake cha Ishema, bado hakijaandikishwa nchini Rwanda.
SHARE
No comments:
Post a Comment