Rais wa Zimbabwe
Robert Mugabe amesema anakubaliana na sera ya Rais wa Marekani Donald
Trump kwamba "Marekani iwe ya Wamarekani".
Bw Mugabe, ambaye ndiye
mara ya kwanza anazungumzia utawala wa Bw Trump, amesema alishangazwa
na ushindi wa kiongozi huyo wa Republican.Hata hivyo, amesema hakutaka pia "Madam Clinton ashinde", akirejelea mgombea wa chama cha Democratic aliyeshindwa uchaguzi wa Novemba mwaka jana Hillary Clinton.
"Lakini vilevile, ukija kwa Donald Trump ambapo anazungumzia uzalendo... Marekani iwe ya Wamarekani - katika hilo, nakubaliana naye. Zimbabwe iwe ya Wazimbabwe," Bw Mugabe amesema, kwenye dondoo ambazo zimechapishwa katika gazeti rasmi la serikali la Herald.
Ameongeza kwamba Bw Trump anafaa kupewa muda wa kudhihirisha uwezo wake.
"Sijui. Mpeni muda. Bw Trump huenda hata labda ataangalia upya vikwazo vilivyowekewa Zimbabwe," Bw Mugabe amesema.
Mahojiano kamili ya Bw Mugabe yanatarajiwa kupeperushwa rasmi kesho jioni kwenda sambamba na maadhimisho ya kusherehekea kiongozi huyo kutimiza miaka 93 tangu kuzaliwa kwake
Bw Mugabe pia amesema anafaa kuendelea kuongoza, kwani watu wengi nchini mwake wanahisi kwamba hakuna mtu anayetosha kuchukua pahala pake.
Kiongozi huyo tayari ameteuliwa na chama tawala cha Zanu-PF kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Bw Mugabe ameongoza Zimbabwe nchi hiyo tangu uhuru mwaka 1980.
SHARE
No comments:
Post a Comment