Mkuu wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma,Bi.Vumulia Nyamonga,akifungua mafunzo ya TPSF mkoani Dodoma
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya TPSF,Bw.Godfrey Sembeye,akiongea wakati wa mafunzo ya wajasiriamali mkoani Dodoma
Mwezeshaji kutoka taasisi ya TPSF Celestine Mkama akitoa mada kwenye mafunzo hayo
Mmoja wa wawezeshaji ,Iringo Ringo akitoa mada kwenye mafunzo hayo
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa na wawezeshaji
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa na wawezeshaji
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa na wawezeshaji
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa na wawezeshaji
……………………………………………………………………………..
Mkuu
wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma,Bi.Vumulia Nyamonga,amewataka
wajasiriamali kutumia elimu ya ujasiriamali inayotolewa na taasisi ya
TPSF kuboresha biashara zao.
Akifungua
mafunzo kwa wajasiriamali wa mkoani Dodoma yaliyofanyika katika ukumbi
wa KKKT mkoani humo,Nyamonga ,alisema kuwa matokeo ya kupata elimu ni
kubadilika hivyo anaamini elimu ya ujasiriamali watakayoipata itasaidia
kuleta tija kwenye biashara zao.
“Nawapongeza
TPSF kwa kazi nzuri mnayofanya kuhakikisha wajasiriamali wanapata ujuzi
unaosaidia kuboresha biashara zao kwa kuziendesha kitaalamu ili
ziwe endelevu na natoa wito kwa wajasiriamali mnaobahatika kuhudhuria
kwenye mafunzo haya kuwauliza masuala mbalimbali wataalamu yanayohusiana
na changamoto mnazokumbana nazo katika biashara ili wataalamu
wawasaidie”
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya TPSF,Bw.Godfrey
Sembeye,alisema kuwa taasisi yake imejikita zaidi kusaidia kukuza
wajasiriamali wadogo kwa kuwa ndio chanzo kikubwa cha ukuaji wa uchumi
hapa nchini hivyo wanatakiwa kusaidiwa ili kuendelea kuchangia pato
hilo.
Simbeye
alisema takwimu zinazonyesha kuwa kundi hilo la Wajasiriamali ni zaidi
ya milioni 3.1 hivyo wanatakiwa kusaidiwa ili kuendelea kuchangia pato
la Taifa.
Alisema kubwa lengo la mafunzo hayo kwa wajasiliamali ni kuwajengea uwezo katika biashara zao ili kuweza kujiendeleza zaidi na kuwasaidia kuongeza mitaji na kuwatafutia masoko ya biashaara zao .
Simbeye alisema taasisi hiyo imekuwa ikitoa elimu ya mafuzo kwa Wajasiliamali kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo njia ya redio,luninga,magazeti na tovuti ya taasisi hiyo.
Alisema mpaka saa elimu hiyo imeishawapatia mafunzo wajasiriamali waliopo katika mikoa ya Geita,Mbeya,Kigoma na Dodoma.
SHARE
No comments:
Post a Comment