Na Mwamvua Mwinyi, Kibiti
KAMANDA wa jeshi la
polisi mkoani Pwani, Boniventure Mushongi, amesema jeshi hilo kwa
kushirikiana na makachero wake linaendelea na msako mkali kuwasaka
waliohusika katika tukio la mauaji lililotokea feb 21 huko Jaribu
Mpakani, kata ya Majawa, Kibiti.
Aidha ameeleza kwamba, taarifa zaidi juu ya matokeo ya msako huo zitatolewa wakati wowote mara baada ya kuwabaini wahalifu hao.
Katika tukio hilo, watu
watatu walipoteza maisha ambapo mmoja kati yao akiwa OC CID Kibiti
baada ya kuuwawa na kundi la watu wanaodhaniwa ni majambazi wakiwa na
silaha aina ya SMG/SAR .
Kamanda Mushongi
alisema tukio hilo limetokea feb 21 majira ya saa mbili usiku ambapo
watu sita walivamia katika kituo cha ukaguzi wa mazao ya misitu na
kuwauwa watu watatu .
Waliouawa ni pamoja na OC CID wilaya ya Kibiti sp.Peter Kubezya ambae alipigwa risasi kwenye kiuno .
Alitaja wengine kuwa ni
Peter Kitundu Mkaguzi wa maliasili kituo cha Jaribu Mpakani na mgambo
aliyekuwa akifanyakazi za ulinzi kwenye kizuizi hicho, Athumani Ngambo .
Kamanda Mushongi alisema wote hao wawili waliuawa kwa kupigwa risasi kichwani na begani na kupoteza maisha papo hapo .
“Upelelezi na operesheni zinaendelea usiku na mchana ili kuhakikisha waliofanya tukio hilo wanapatikana “alisema.
Alifafanua ,katika eneo
la tukio kulikutwa pikipiki mbili namba MC 853 AHH aina ya Toyo na MC
799 aina ya Sunlg na kipeperushi chenye ujumbe wa kitisho .
SHARE
No comments:
Post a Comment