Majeshi ya serikali ya Iraq yameukomboa uwanja wa ndege wa mji wa
Mosul, hatua ambayo ni muhimu katika mashambulio ya majeshi hayo yenye
lengo la kuwatimua magaidi wanaojiita Dola la Kiislamu IS kutoka
Magharibi mwa mji wa Mosul. Mapambano hayo yalichukua muda wa saa nne.
Majeshi ya Iraq yalisaidiwa na ndege za kivita za Marekani. Mapambano ya
kuukomboa mji wa Mosul yalianza mnamo mwezi wa Oktoba mwaka uliopita na
tangu wakati huo magaidi wanaojiita Dola la Kiislamu walifurushwa
kabisa kutoka sehemu ya Mashariki ya mji huo. Hata hivyo kwa mujibu wa
taarifa, wapiganaji hao wa IS wenye itikadi kali waliendelea na
mapambano kwa kutumia mizinga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment