Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson anayeongozana na
waziri wa mambo ya ndani John Kelly wamekutana na rais wa Mexico Enrique
Peña Nieto pamoja na mawaziri wa mambo ya nje Luis Videgaray na waziri
wa fedha Jose Antonio Meade. Tillerson amesema Marekani na Mexico
zinaunganishwa na msimamo wa pamoja juu ya kudumisha sheria na utulivu
kwenye mpaka wa nchi zao. Waziri wa mambo ya nje wa Mexico kwenye
mkutano na waandishi wa habari alieleza kwamba tafauti baina ya nchi
yake na Marekani bado zinaendelea lakini sasa njia mpya imetafutwa.
Uhusiano kati ya Marekani na Mexico umekwaruzika tangu kuingia
madarakani kwa rais Donald Trump aliyeahidi kukomesha wahamiaji haramu
kuingia nchini Marekani kutokea Mexico.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment