Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na Mkuu wa Masoko Kanda ya Afrika Mashariki,Roberto Jarrin (kulia) akifafanua jambo kwa wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika wanaosoma Programu ya utawala wa Biashara ya Chuo cha Swedish Institute wakati walipofanya ziara ya mafunzo katika kiwanda cha bia cha Ilala jijini Dar es salaam
Meneja wa kiwanda cha TBL Ilala akiongea na wanafunzi kuhusu mifumo ya uendehaji bora wa viwanda
Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group na Mkuu wa Masoko Kanda ya Afrika Mashariki,Roberto
Jarrin akibadilishana mawazo na baadhi ya wanafunzi na wakufunzi kutoka
Swedish Institute
Mmoja
wa wanafunzi anayesoma katika Programu ya Biashara na Utawala ya
Swedish Institute Ng’winula Kingamkono (kushoto) akiuliza swali kwa
watendaji wa TBL Group
Mtaalamu
wa upishi wa bia kiwanda cha Ilala jijini Dar es Salaam, Calven
Naiman,akiwaeleza wanafunzi hao jinsi upishi wa bia unavyofanyika
Baadhi ya wanafunzi kutoka taasisi ya Swedish Institute wakibadilishana mawazo wakazi wa ziara hiyo ya mafunzo
Meneja wa Kiwanda cha bia cha TBL Group Ilala jijini Dar es Salaam, Calvin Martin,akiwaongoza wanafunzi kutembelea maeneo ya kiwanda
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa mmoja wa wanafunzi ,Eric Muthomi,kwa niaba ya wenzake
……………………………………………………………………..
–Asema mafanikio ya kampuni yake yanaletwa na wafanyakazi wenyewe
Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group na Mkuu wa Masoko kanda ya Afrika Mashariki,Roberto
jarrin,amesema uanzishwaji wa biashara na uwekezaji unaofanywa kwenye
nchi za Afrika unatoa mchango wa kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira
hivyo kuna umuhimu mkubwa kuhakikisha kunakuwepo wataalamu wa kubuni na
kuendesha mifumo ya kisasa ya biashara ili biashara hizo zizidi kukua
na kuwa endelevu.
Roberto aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akiongea na wafanyakazi kutoka nchi mbalimbali za Kiafrika ambao wanahudhuria mafunzo ya ukuzaji wa biashara endelevu chini
ya mpango ujulikanao kama Swedish Institute Management Programme
unaolenga kuwajengea uwezo wa biashara na utawala vijana wasomi kutoka
barani Afrika walipotembelea kiwanda cha TBL cha Ilala jijini Dar es
Salaam.
Alisema biashara yoyote inayoendeshwa kwa kufuata misingi ya kitaalamu ni lazima ipate mafanikio na kuwa endelevu “Biashara
ikiendeshwa kwa misingi ya kitaalamu inakua kwa haraka na kuchangua
kukuza uchumi wa nchi,kuongeza wigo wa ajira za moja kwa moja na zisizo
za moja kwa moja,kuchangia pato kubwa kwa serikali kwa njia ya kulipa
kodi na kunufaisha jamii kwa namna mbalimbali”.
Aliwaeleza wanafunzi hao kuwa TBL Group kupitia viwanda vyake
vilivyopo kwenye mikoa mbalimbali nchini kwa kiasi kikubwa imekuwa
ikizingatia kuendesha shughuli zake kwa kufuata misingi bora ya
uendeshaji biashara ambayo kwa kiasi kikubwa imewezesha kampuni kupata
mafanikio mengi na kuwa kioo cha uwekezaji bora ambapo watu kutoka
sehemu kadhaa wamekuwa wakitembelea viwanda vyake kwa ajili ya kujifunza
mifumo ya uzalishaji bora wenye tija na ufanisi.
“Kampuni
ya TBL Group imekuwa ikifanya vizuri katika maeneo mbalimbali ikiwemo
kuchangia pato la taifa kwa njia ya kulipa kodi,utunzaji wa
mazingira,kutoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja
kupitia mtandao wa biashara zake,kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa
wafanyabiashara wadogo inaoshirikiana nao,kuendesha kampeni ya unywaji
wa kistaarabu kwenye jamii,kuwezesha wakulima ambao wanaiuzia malighafi
na imekuwa kinara wa kutekeleza kanuni bora za ajira ambapo imekuwa
ikishikia rekodi ya kupata tuzo ya Mwajiri bora inayotolewa na Chama cha
Waajiri nchini (ATE)”.
Roberto
alisema kuwa mafanikio haya hayatokani na kufuata mifumo bora ya
uzalishaji pekee bali ni kuwa na wafanyakazi wenye vipaji vikubwa na
taaluma mbalimbali ambao wanafanya kazi kwa kujituma wakati huohuo
kampuni ikiwa inawapatia motisha na mafunzo ya kwa mara ili kuhakikisha wakati wote wanakwenda na wakati sambamba na mabadiliko ya teknolojia yanayotokea siku hadi siku.
Aliwaeleza kuwa TBL Group itaendelea kufanya kazi sambamba na serikali,taasisi zingine na wananchi kwa ujumla kwenye jamii kuhakikisha maendeleo
endelevu yanapatikana na aliipongeza taasisi ya Swedish Institute kwa
kubuni programu ya kuwanoa Vijana wasomi katika mitaala ya uendeshaji
biashara kwa mifumo ya kisasa yenye lengo la kuleta ufanisi na kukuza
sekta mbalimbali za biashara.
Kwa upande wake Meneja wa mafunzo hayo
kutoka taasisi ya Swedish Institute,Matilda Axelsson,alisema ziara ya
mafunzo waliyofanya kiwandani hapo imewawezesha wanafunzi wake kupata
maarifa kuhusiana na mifumo bora ya uendeshaji wa viwanda kwa tija.
Alisema
kuwa taasisi hiyo tangia ianze kutoa mafunzo ya kibiashara na utawala
barani Afrika tangia mwaka 2008 imepata mafanikio makubwa ambapo vijana
wasomi kutoka nchi mbalimbali wamekuwa wakijiunga kwenye Programu zake
za kibiashara kwa ajili ya kunolewa na kuwaanda kuwa waendeshaji wa
biashara wazuri “Tutazidi
kujipanga kuhakikisha vijana wengi wasomi wanapata fursa za kuhudhuria
mafunzo haya na natoa wito kwa waajiri kuwadhamini wafanyakazi wao
kupata mafunzo zaidi ili kuleta ufanisi wa kibiashara kupita raslimali
watu”.Alisema.
SHARE
No comments:
Post a Comment