Utafiti uliofanywa na wataalamu kutoka chuo cha Imperial College
umegundua kuwa umri wa kuishi kwa watu katika mataifa yanayoendelea
unazidi kuongezeka. Kwa mujibu wa utafiti wa chuo hicho cha mjini
London, Uingereza ambao leo umechapisha takwimu zake katika jarida la
The Lancet, umri wa kuishi katika baadhi ya nchi hivi karibuni unaweza
ukazidi miaka 90. Wakati huo huo, utafiti huo umegundua kuwa pengo kati
ya wanaume na wanawake pia linapungua na kwamba umri wa juu wa kuishi
uko nchini Korea Kusini. Watafiti hao wamesema kuwa ifikapo mwaka 2030
umri wa kuishi kwa wanawake wa Korea Kusini unaweza ukazidi miongo
minane. Mataifa ambayo miongoni mwake wanaume wataishi kwa muda mrefu
hadi kufikia umri wa miaka 84 ifikapo mwaka 2030, ni Korea Kusini,
Australia na Switzerland.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment