Kaimu
Meneja Mkuu wa TDL,Devis Deogratius,akiongea na waandishi wa
habari,(katikati )ni Afisa Mwandamizi wa Masoko wa kampuni hiyo,George
Kavishe
Mfano wa mwonekano wa vifungashio vipya vya vinywaji vya konyagi vitakavyokuwa
………………………………………………………………………………………….
-Kuomba kibali cha kuondoa bidhaa zake zenye vifungashio vya mifuko ya Plastiki zilizopo kwenye masoko
Tanzania Distilleries Limited (TDL),kampuni tanzu ya TBL Group imeunga mkono jitihada za serikali kupiga marufuku ufungaji wa pombe kwa kutumia mifuko ya plastiki nchini.
Kaimu
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo,Devis Deogratius,amesema kampuni yake
itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali kupambana na matumizi ya
vifungashio vya mifuko ya plastiki na tayari iko katika mchakato wa
kuacha kuvitumia kufungia bidhaa zake badala yake itatumia vifungashio vya kisasa vilivyotengenezwa kwa malighafi ya kioo.
“Tunajipanga
kuhakikisha bidhaa zetu zote ambazo zinapatikana sokoni zikiwa
zimefungwa kwenye mifuko ya Plastiki kuhakikisha sasa zinapatikana
katika vifungashio vya kioo”.Alisema.
Kuhusiana
na suala la vijana wadogo kununua na kutumia bidhaa zenye kilevi
zinazopatikana kwa urahisi na kwa gharama nafuu,Deogratius,amesema kuwa
TDL itasimamisha kuzalisha pombe kwenye kifungashio chenye ujazo wa 50ml
badala yake itaingiza kinywaji kitakachouzwa kwa shilingi 500.
Aliongeza
kuwa kuna haja ya wadau mbalimbali nchini kushirikiana kuhakikisha
sheria ya kununua na kutumia vinywaji vyenye kilevi kwa watoto wadogo
chini ya umri wa miaka 18 inatekelezwa “Ili
sheria hii ifanye kazi wadau wote tunapaswa kushirikiana na mamlaka
zinazohusika kuhakikisha kila mtu anayefikisha umri wa miaka 18
anapatiwa kitambulisho cha taifa ambacho mnunuzi wa vinywaji vyenye
kilevi atakayetiliwa mashaka ya umri atapaswa akionyeshe kabla ya kuhudumiwa kwenye sehemu zinazouzwa vinywaji vyenye kilevi.”Alisema.
Deogratius
pia alisema kuwa TDL itaomba kibali kutoka mamlaka husika cha kupata
muda wa kuondoa bidhaa zake zilizofungwa kwa mifuko ya plastiki zilizopo
kwenye masoko ambazo ni Konyagi, Zanzi Cream Liqueur na Valeur Superior
Brandy.
SHARE
No comments:
Post a Comment