Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Katesh
wilayani Hanang, Februari 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa
akimkabidhi zawadi ya Shilingi 500,000/= mzee Giloya Semhonda ikiwa ni
shukurani kwa usimamizi wake mzuri wa ujenzi na ukarabati wa madarasa ya
shule ya msingi ya Mogitu wilayani Hanang baada ya uzindu madarasa hayo
Februari 21, 2017. Fedha hizo zilitolewa na Mkuuu wa Mkoa wa Manyara,
Dkt. Joel Bendera.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiwa katika apicha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Msingi ya Mogitu
wilayani Hanang baada ya kuzindua madarasa ya shule hiyo, Februari 21,
2017. Watatu kulia ni Mbunge wa Hanang, Dkt. Mary Nagu. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akitazama ngoma ya asili ya kabila la Wanyaturu kabla ya kuhutubia
mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Katesh wilayani
Hanang Februari 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizindua madarasa ya Shule ya Msingi ya Mogitu wilayani Hanang Februari
21, 2017. Kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Eliakim
Maswi na wapili kulia kwake ni Mbunge wa hanang, Dkt. Mary Nagu. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
SHARE
No comments:
Post a Comment