Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine ameahidi kuwafukuza
nchini mwake watu ambao amewaita wahalifu na pia ameahidi kujenga ukuta
haraka hata kabla ya wakati uliopangwa katika mpaka wa Marekani na
Mexico. Rais Trump aliyasema hayo kwenye mkutano wa wanaharakati wa
kisiasa wa jumuiya ya wahafidhina ya CPAC katika jimbo la Maryland.
Trump amevilaumu vyombo vya habari vya Marekani, na amewaambia wajumbe
kwenye mkutano huo unaofanyika kila mwaka kwamba hataomba radhi kwa
kuyaweka mbele maslahi ya Wamarekani. Trump aliwaeleza wajumbe kwenye
mkutano huo kwamba anazilaumu nchi za Ujerumani, Sweden na Ufaransa
jinsi zinavyosimamia vibaya maswala ya uhamiaji. Tangu Trump
alipoapishwa mwezi mmoja uliopita, Marekani imekumbwa na maandamano
kupinga maswala kama ya uhamiaji, sekta ya afya pamoja na uhusiano wake
na Urusi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment