Polisi nchini Afrika Kusini walitumia risasi za mipira, gesi ya kutoa
machozi na maji ya kuwasha ili kuwatawanya watu waliokuwa wanafanya
maandamano ya kuwapinga wahamiaji mjini Pretoria. Polisi pia walitumia
helikopta iliyoruka katika upeo wa chini ili kuwatenganisha wazaliwa na
wahamiaji waliokuwa wanapambana. Hata hivyo Rais wa Afrika Kusini Jacob
Zuma amedai kwamba maandamano hayo yalikuwa ya kupinga uhalifu na siyo
dhidi ya wageni lakini rais Zuma alilaani vitendo vya matumizi ya nguvu
na vitisho walivyofanyiwa wahamiaji nchini mwake. Mapema wiki hii,
wenyeji wa nchi hiyo waliokuwa na hasira waliwashambulia wageni kutoka
Nigeria na pia walipora maduka ya Wasomali, Wapakistani na ya wahamiaji
wengine katika miji ya Pretoria na Johannesburg. Wenyeji wanadai kwamba
wageni wanachukua nafasi za ajira na wanashiriki katika vitendo vya
ukahaba.
DW
DW
No comments:
Post a Comment