Kamishna Jenerali wa
Magereza, Dkt. Juma Malewa(meza kuu) akiongea na ujumbe kutoka Chuo cha Ulinzi wa Taifa. Ujumbe huo wa Washiriki wa
Mafunzo wametembelea Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika ziara yao
ya Mafunzo kuhusu Uendeshaji wa shughuli za Magereza hapa nchini leo Februari
23, 2017.
Kamishna Jenerali wa
Magereza, Dkt. Juma Malewa akisisitiza jambo kwa Maafisa kutoka Chuo cha Ulinzi wa
Taifa(hawapo pichani) walipotembelea Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza
katika ziara yao ya Mafunzo kuhusu Uendeshaji wa Jeshi hilo.
Mkuu
wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akitoa
utambulisho mfupi kwa Wakufunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi
Tanzania alioambatananao katika ziara ya mafunzo.
Baadhi ya Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia mazungumzo hayo kama inavyoonekana
katika picha
Wakufunzi
na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania wakipata
maelezo mafupi toka kwa Wataalam wa Jeshi la Magereza walipofanya ziara ya
mafunzo katika Kiwanda
Mkuu
wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali Yacoub Mohamed
akijalibisha kiti Maalum cha kunesa kilichotengenezwa kwa ustadi mkubwa katika
Kiwanda cha Seremala Gereza Kuu Ukonga, Dar es Salaam kama inavyoonekana katika
picha.
Kamishna Msaidizi wa
Magereza, Charles Novart akiwasilisha mada yake ya uchokozi kuhusu
Historia na Muundo wa Jeshi la Magereza mbele ya Wakufunzi na Wanafunzi
Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania(hawapo pichani).
Wakufunzi
na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania wakifuatilia
mijadala katika uwasilishaji wa mada kuhusu Mafanikio na Changamoto katika
uendeshaji wa Jeshi la Magereza katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza,
Ukonga Dar es Salaam leo Februari 23, 2017.
Mkuu
wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania, Meja Jenerali Yacoub Mohamed akikabidhi zawadi kwa Naibu
Kamishna wa Magereza, Edith Mallya(kushoto) mara baada ya uwasilishaji wa mada kuhusu
Mafanikio na Changamoto katika uendeshaji wa Jeshi la Magereza katika Ukumbi wa
Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga Dar es Salaam leo Februari 23, 2017.
Kamishna
Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa(wa sita toka kulia)akiwa katika picha ya
pamoja na Maafisa Wakufunzi na Wanafunzi Washiriki kutoka Chuo cha Taifa cha
Ulinzi Tanzania walipofanya ziara ya mafunzo waliyoifanya katika Jeshi la
Magereza(wa nne toka kushoto) ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania,
Meja Jenerali Yacoub Mohamed(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
SHARE
No comments:
Post a Comment