Mwakiishi
wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini
Tanzania ,Alvaro Rodriguez,akishirikiana na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano
wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki ,Balozi Celestine Mushy wamezindua vyoo 10 vilivyojengwa
katika shule za msingi 10 wilayani Moshi.
Ujenzi huo ulifanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya uwapo wa Umoja wa Mataifa.
Wakati
wa maadhimisho hayo pia wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa walifanya
shughuli mbalimbali mkoani Kilimanjaro za kusaidia maendeleo ikiwamo
hifadhi ya mazingira na usafi.
Katika
kuhakikisha kwamba shule zinakuwa na UNDP Tanzania ilisaidia mkoa wa
Kilimanjaro Sh Mil 510 kujenga vyoo vya kisasa katika shule za msingi
10 ili kusaidia kuezesha usafi kwa wanafunzi na walimu wao.
Hadi
kufikia sasa jumla ya matundu 178 yamejengwa katika shule 10 ambapo
matundu 104 ni kwa ajili ya wasichana na 74 kwa ajili ya wavulana.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Mwakilishi makzi wa UNDP.Alvaro Rodriguez
alipongeza mradi huo na ushirikiano uliokuwepo kati ya serikali ,wao na
shule ikiwa ni hatua moja ya maendeleo endelevu kwa kuboresha mazingira
ya usafi kwa wanafunzi wa kike na wa kiume katika masomo yao na hivyo
kuimarisha safari ya kuelekea malengo ya dunia ya 2030.
Alisema
kutokuwepo kwa mazingirabora ya usafi ni chanagamoto kubwa kwa
wanafunzi na hali hiyo inawaathiri sana wanafunzi wa kike.
Rodriguez
alisema kutokana na kujengwa kwa vyoo hivyo wanafunzi ,walimu na walezi
sasa watakuwa na kazi pekee ya kuhakikisha kwamba wanatoa elimu bora .
“Watoto
wa kike watakuwa na changamoto chache zaidi za mahudhurio shuleni na
wakati huo huo masUala ya usafi yatakuwa yameboreka na hivyo kuwa na
wanafunzi na familia zenye siha njema.”alisema Rodriguez.
Kwa
upande wake Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika wizara ya
Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Balozi Celestine Mushy
amepongeza kwa msaada huo na kuutaka Umja wa MAtaifa kuendelea kutoa
msaada kwa shule zenye mahitaji makubwa kuhakikisha kwamba malengo ya
dunia yanayohusiaa na usafi ,mazingira na maji safi yanafanikiwa ifikapo
mwak 2030.
Naye
mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba pamoja n kuishukuru UNDP kwa
kazi nzuri waliyofanya pia alizitaka jumuiya za maeneo yaliyojengewa
vyoo kuiliki msaada huo kwa kuhakikisha wanaitumia na hivyo kuisadia
kufikia malengo ya dunia 2010.
Mwakilishi
wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini
,Alvaro Rodriguez pamoja na Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba
wakizindua rasmi vyoo vilivyojengwa katika shule za msingi 10 wilayani
Moshi za kufadhiliwa na UNDP.
Mwakilishi
wa Shirika la Mpango wa Maendeelo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini
Alavaro Rodriguez pamoja na Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba
wakitizama vyoo vilivyojengwa na UNDP katika shule ya Msingi Mandela.
Mkuu
wa Idara ya Ushirikino wa Afria Mashariki ,Balozi Celestine Mushy
(katikati) akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba
(Kulia) kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya mara
baada ya kuzinduliwa kwa vyoo katika shule za msingi za Mandela na
Azimio.
Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeelo la Umoja wa Mataifa (UNDP)
nchini Alvaro Rodriguez na ujumbe wake wakiangalia vyoo vya kisasa
vilivyojengwa katika shule 10 katika manispaa ya Moshi na Manispaa ya
Moshi.
Jengo la Choo kipya na cha kisasa kilichojengwa katika shule za Msingi za Azimio na Mandela vilivyojengwa na UNDP.
Choo
maalumu kwa ajili ya walemavu kilichojengwa katika vyoo vipya
vilivyojengwa na UNDP katika shule ya msingi 10 za Msingi wilayani
Moshi.
Mkuu
wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi
rasmi wa Vyoo 10 zilizojengwa katika shule za msingi 10 za wilaya ya
Moshi.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya akiteta jambo na Mwakilishi wa
Shirika la Mpango wa Maendeelo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro
Rodriguez wakati wa uzinduzi wa vyoo katika shule za msingi.
Mwakilishi
wa Shirika la Mpango wa Maendeelo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini
Alvaro Rodriguez akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Majengo ya
vyoo katika shule 10 za Msingi,Moshi.
Mkuu wa Idara ya Ushirikino wa Afria Mashariki ,Balozi Celestine Mushy akizungumza katika uzinduzi huo.
Wanafunzi
katika shule za Msingi za Azimio na Mandela wakitoa burudani za nyimbo
na Ngoma wakati wa uzinduzi rasmi wa Vyoo katika shule za msingi za
Azimio na Mandela.
Mkuu
wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba pamoja na Mwakilishi wa Shirika la
Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini ,Alvaro Rodriguez
wakiwa katika picha za pamoja na viongozi wengine pamoja na kamati ya
shule hizo.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba pamoja na Mwakilishi wa Shirika la
Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini ,Alvaro Rodriguez
wakiwa katika picha za pamoja na wanafunzi wa shule za Azimio na Mandela.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
SHARE
No comments:
Post a Comment