Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa
PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto), akizungumza jambo na Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt. Charels Kimei, wakati wa uzinduzi wa
ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili ambapo CRDB sasa itawakopesha
Wanachama wa PSPF kwenye maeneo ya elimu, viwanja na pesa za kuanzia
maisha kwa watumishi wa serikali. Uzinduzi huo umefanyika Februari 27,
2017 makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam.
Bw. Mayingu akitoa hotuba yake kuelezea
ushirikiano huo ambao lengo lake kubwa ni kupanuan wigo wa huduma kwa
Wanachama wa Mfuko huo
Dkt. Charles Kimei, akitoa hotuba yake kueleza jinsi benki yake ilivyofurahishwa na ushirikiano huo
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, akitoa hotuba ya ukaribisho
Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa
Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, (katikati), na Msaidizi
Mtendaji wa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Bw.Keneth Kasigila,
wakimsikiliza Mkurugenzi wa Wateja wa Mashirika wa CRDB, Bw.Goodluck
Nkini, (kushoto), wakati wa hafla hiyo.
Bw. Mayingu, (kushoto) na Dkt. Kimei, wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya kufanyika kwa uzinduzi huo
Viongozi wa juu wa PSPF, wakipiga makofi wakati wa hafla hiyo
Baadhi ya maafisa wa CRDB waliohudhuria hafla hiyo
Baadhi ya maafisa wa PSPF
Baloziwa PSPF, Mrisho Mpoto, (kushoto), akiongoza kuimba wimbo wa taifa
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dkt.
Charles Kimei, (kushoto) na Balozi wa PSPF, Bw. Mrisho Mpoto (katikati),
wakimsikiliza Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi kabla
ya kuanza kwa hafla hiyo
Baadhi ya maafisa wa PSPF waliohudhuria hafla hiyo
Mkurugenzi wa Mipangona Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, akitoa neno la shukrani mwishoni mwa hafla hiyo
Anna Lukando wa kampuni ya Ardhi Plan
Limited, yenye ushirikiano na PSPF, akizungumzia jinsi wanachamawa Mfuko
huo wanavyoweza kufaidika naupatikanajiwa viwanja vilivyopimwa kisheria
Maafisa wa PSPF na CRDB wakifuatilia hafla hiyo
Maafisa wa CRDB |
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa
Hiari, (PSS), wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Bi.Mwanjaa Sembe, (kulia),
akimkabidhi kadi ya kujiunga na mpango huo, mfanyakazi wa CRDB, Bi.
Fausta Urassa
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw.
Abdul Njaidi, (kulia), akimkabidhi kadi ya kujiunga na mpango wa
uchangiaji wa hiari (PSS), mfanyakazi wa CRDB, Bw.Alfred Kessy.
Balozi wa PSPF, Bw. Mrisho Mpoto, (kulia),akimkabidhi kadi ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), mfanyakazi wa CRDB, Bi. Flora Munisi. |
Picha ya pamoja ya wanachama wapya wa PSPF na maafisa wa Mfuko huo akiwemo Balozi Mpoto |
Uzinduzi rasmi ukifanyika
SHARE
No comments:
Post a Comment