Katibu
wa Baraza la Watoto Shehia ya Kiembesamaki Zulfa Mohd Masanja akisoma
risala wakati wa sherehe za ufunguzi wa Baraza hilo zilizofanyika Tawi
la CCM Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi ‘B’.
Watoto
wa Baraza la watoto Shehia ya Kiembesamaki wakionyesha igizo lenye
maudhui ya udhalilishaji watoto wakati wa sherehe za kulizindua baraza
hilo.
Mgeni
rasmi katika uzinduzi wa Baraza hilo, Mwakilishi wa Jimbo la
Kiembesamaki ambae pia ni Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo
akifuatilia maonyesho ya watoto wa Baraza hilo (kulia) Mwenyekiti wa
Bodi ya ushauri ya watoto Zanzibar Mundhir Hamdan Said.
Mwenyekiti
wa Baraza la Watoto Shehia ya Kiembesamaki Bimkubwa Haji Hassan
akimkaribisha mgeni rasmi kuzindua Baraza la watoto la shehia hiyo.
Mwakilishi
wa Jimbo la Kiembesamaki ambae ni Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo
akizindua Baraza la Watoto wa Shehia ya Kiembesamaki katika sherehe
zilizofanyika Tawi la CCM Kiembesamaki.
Baadhi
ya watoto wa Shehia ya Kiembesamaki wakimsikiliza Mwakilishi wao
Mahmoud Thabit Kombo wakati wa uzinduzi wa Baraza lao kwenye sherehe
zilizofanyika Tawi la CCM Kiembesamaki Wilaya Magharibi ‘B’.
Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.
SHARE
No comments:
Post a Comment