Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru
Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki la Watakatifu Wote Jimbo la Mtwara
Fr. Patrick Mwaya mara baada ya mahubiri katika Kanisa hilo Jumapili.
Rais Dkt. Magufuli amechangia Kanisa hilo Mifuko 200 ya Saruji kwa ajili
ya kuendeleza kazi ya ujenzi wa uzio Kanisani hapo.
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasalimia Waumini wa Kanisa Katoliki la Watakatifu Wote Jimbo la
Mtwara mara baada ya mahubiri.
Kaimu
Katibu wa Rais Ikulu, Ngusa Samike(Kushoto) akimkabidhi Askofu Msaidizi
wa Kanisa Katoliki la Watakatifu Wote Jimbo la Mtwara Fr. Patrick Mwaya
mifuko 200 ya Saruji ili kutimiza Ahadi ya Rais aliyoitoa kanisani
hapo.
Kaimu
Katibu wa Rais Ikulu, Ngusa Samike(Kushoto) akimkabidhi fedha kiasi cha
Shilingi Milioni 35 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ili
kutekeleza ahadi aliyoitoa Rais wakati alipopita katika Kijiji cha
Somanga na Mnonela. Katika kijiji cha Somanga Rais Dkt. Magufuli
aliahidi kuchangia kiasi cha Shilingi Milioni 20, kwa ajili ya ujenzi wa
Kituo cha Afya na kwa upande wa Mnonela aliahidi kiasi cha Shilingi
milioni 15 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa Kituo cha Afya.
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi akisaini kuthibitisha kupokea kiasi
hicho cha fedha ambazo ni utekelezaji wa ahadi za Rais Dkt. Magufuli
wakati alipofanya ziara mkoani humo.
Rais
Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika kituo cha Afya mnonela
katika Jimbo la Mtama ambapo aliahidi kuchangia kiasi cha fedha Shilingi
Milioni 15 ambazo tayari Mkuu wa Mkoa wa Lindi ameshakabidhiwa.
PICHA NA IKULU
SHARE
No comments:
Post a Comment