Msanii
wa Bongo Flava na Dancer maarufu, Msami ameeleza ulipoanzia utaratibu
wa wasanii kujiita Simba jina ambalo Diamond Platnumz amekuwa
akilitumia.
Muimbaji
huyo ameeleza kuwa wakati wanaenda kushiriki mashindano ya kudansi yeye
na Mose Iyobo walipenda kutumia jina hilo hasa pale wanapokutana na
dancer wenye uwezo wa chini zaidi yao.
“I
think hata jina la Simba lilianzia kwa mimi na Mose, mimi nilikuwa
nakutana na Mose ananiita Simba, namuita yeye Simba that time Diamond
alikuwa anacheza lakini sio sana,”
“Diamond
ni mtu ambaye alikuwa anakuja kwenye mashindano ya dance. Hata nikienda
kufundisha kule Wasafi Mose ananiitaga Simba, Diamond naye akawa
ananiita Simba na mimi nikawa namuita Simba mpaka baadae limekuwa kubwa
lakini lilivyoleta stori nyingi huwezi kuibuka na kusema utaonekana kuna
vitu unahitaji,” amesema Msami.
Msami kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘So Fine’ ambayo amemshirikisha Chemical.
SHARE
No comments:
Post a Comment