Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi
na wafanyakazi wa kiwanda cha
kutengeneza vigae (Tiles) cha
Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani mara baada
ya kuweka jiwe la msingi leo wilayani Mkuranga, Pwani, Machi 2, 2017.(PICHA NA
FRANK
SHIJA – MAELEZO).
NA
BENJAMIN SAWE, MKURANGA
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli amezuia usafirishaji
wa mchanga wa madini kwenda kuuchenjua nje ya nchi akitaka shughuli hizo
zifanyike nchini.
Akizungumza
na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza vigae
cha Tanzania Goodwill Ceramic Rais, Magufuli alisema uchenjuaji wa mchanga wa
madini nje ya nchi kunaikosesha Serikali mapato ikiwa ni pamoja na wizi madini
hayo.
”Ndio
maana nilikataa kusaini mkataba wa EPA kwa sababu kupitia mkataba huo, ni
vigumu kwa kampuni za Tanzania kushinda zabuni katika nchi za Ulaya lakini ni
rahisi kwa kampuni za Ulaya kushinda zabuni Tanzania kutokana na kukomaa
kiteknolojia, na hata zinaposhindanishwa kampuni za Tanzania na Ulaya ni rahisi
kwa kampuni za Ulaya kushinda, jambo litakalochangia kuua kampuni zetu”alisema
Rais Magufuli.
Alisema
Tanzania ni mwananchama wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo
ya Kusini mwa Afrika SADC hivyo kujengwa kwa kiwanda hicho
kutapelekea kiwanda hicho kunufaika kiuchumi.
Rais
Magufuli alisema kwa muda mrefu wawekezaji wamekuwa wakisafirisha malighafi za
Tanzania nje ya nchi kwa ajili ya uzalishaji na kupelekea wananchi kutumia bidhaa
zisizo na ubora.
Katika
uwekaji wa jiwe la msingi wa Kiwanda hicho Mheshimiwa Magufuli alisema imefika
wakati kwa Tanzania kuuza bidhaa zinazozalishwa viwandani na kuachana na
kusafirisha malighafi nje ya nchi kwa ajili ya uzalishaji.
Katika
hatua nyingine Rais John Pombe amesema Serikali yake haina chakula cha kuwapa
wananchi wanaopatwa na tatizo la njaa badala yake amewataka wananchi
kufanyakazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kuzalisha chakula cha kutosha.
Awali
akitoa salamu zake kwa Mheshimiwa Rais, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Biashara Dkt. Adelhelm
Meru amesema kujengwa kwa kiwanda hicho ni faida kwa uchumi wa mwananchi mmoja
mmoja na Taifa kwa ujumla.
Nae Balozi wa Tanzania nchini Mhe.
Lu Youqing alisema
Serikali
ya China kwa sasa iko katika mkakati wa kuhamishia viwanda vyake vingi barani
Afrika na imeamua kuichagua Tanzania kuwa moja kati ya nchi watakazohamishia
viwanda hivyo kutokana na kuridhishwa na dhamira inayoonyeshwa na serikali
katika kuleta maendeleo.
Alisema
China inatambua mchango mkubwa wa Tanzania katika harakati za kujikomboa hivyo
itaendelea kuiunga mkono kuhakikisha inafikia uchumi mzuri.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe mara
baada ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic
Tiles Ltd. kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani leo.Kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo
la Mkuranga Abdallah Ulega, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, Balozi
wa China nchini Dkt. Lu Youqing, Mkurugenzi
Mtendaji wa Kiwanda cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd Fang Habibi na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm
Meru(wapili kushoto).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha
ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic
Tiles Ltd mara baada ya kuweka jiwe la msingi leo Wilayani Mkuranga, Pwani.
Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 8000 za Vigae kwa
siku.Kushoto kwake ni Balozi wa China nchini Tanznia Dkt.Lu Youqing na kulia
kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm
Meru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru (kulia) akimsikiliza
kwa makini Naibu Mkurugenzi wa kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic
Tiles Ltd, Robin Huang (kushoto) wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la
kiwanda hicho leo Wilayani, Mkuranga. Katikati ni Mmoja wa wafanyakazi wa
kiwanda hicho jina lake halikupatikana.
SHARE
No comments:
Post a Comment