Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Ubalozi wa Kuwait nchini umekabidhi visima vinne katika shule za msingi Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Shule za Msingi zilizopata visima hivyo ni Yombo, Umoja , Mwale pamoja na Bwawani. Akizungumza
wakati wa kukabidhi visima hivyo, Balozi wa Kuwait , Jasem Al-Najem
amesema kuwa wanatambua umuhimu wa maji ndiyo maana wameona umuhimu wa
visima hivyo katika shule hizo.
Amesema
wataendelea kutoa misaada hiyo kutokana na mahitaji yaliyopo katika
jamii kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Kuwait.
Al-Najem
amesema kuwa wameweza kuchimba visima 16 vyenye thamani ya Dola za
Kimarekani 63,000 na watu wengine waweze kujitokeza kusaidia jitihada
mbalimbali.
Ubalozi huo pia umekabidhi dawa za binadamu katika Hospitali ya Amana zenye thamani sh.milioni tatu.
Balozi
wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akizundua kisima cha maji safi katika
shule ya Msingi Yombo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa
Red Cresene , Anwari Abdallah Al-Hasawi.Picha na Emmanuel Massaka,
Globu ya Jamii.
Balozi
wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem kushoto na Naibu Mkurugenzi wa Red
Cresene , Anwari Abdallah Al-Hasawi wakinywa maji mara baada kuzindua
kisima katika shule ya msingi Yombo, jijini Dar es Salaam.
Afisa
Elimu, Elimu ya Watu Wazima wa Manispaa ya Ilala , Hamisi Mlangala
akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa visima ambapo alishukuru msaada
huo.
Balozi
wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akikabidhi dawa kwa Mganga Mkuu
Msaidizi wa Hospitali ya Amana, Amimu Kilomoni, jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini , Jasem Al-Najem akitembelea Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.
Balozi
wa Kuwait nchini , Jasem Al-Najem akimsikiliza Mganga Mkuu Msaidizi wa
Hospitali ya Amana, Amimu Kilomoni leo jijini Dar es Salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment