Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa hiyo
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo (Aliyesimama) Boniface Jacob akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa hiyo, Kushoto kwake ni Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo na kulia
ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo Ramadhan Kwangaya
Wenyeviti
wakisikiliza kwa makini maelekezo mbalimbali wakati wa kikao cha kazi
kilichoendeshwa na Mwenyekiti wa kikao hicho Mhe Boniface Jacob ambaye
ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo (Picha zote na Nassir Bakari)
Pichani ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo wakati wa kikao
kutoka kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo Ramadhan Kwangaya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo na Afisa Utumishi wa manispaa ya Ubungo Ndg Ally Juma akishauri jambo wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa hiyo
Usikivu ni jambo la busara kikaoni
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob akizungumza wakati wa kikao cha kazi na Wenyeviti wa Manispaa ya Ubungo.
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amewataka
wenyeviti wa Mitaa iliyopo katika Manispaa hiyo kutumia vyema nafasi zao
za uongozi kwa kuwatumikia wananchi kwa haki huku akiwasihi kuishauri
serikali katika majukumu yake ili kuwa na maendeleo chanya katika maeneo
yao sawia na kupunguza lawama za mambo yaliyopita ili kuwa na Manispaa
imara yenye ukusanyaji mzuri wa mapato.
MD
Kayombo amewasihi wenyeviti hao kuwa na mahusiano mazuri baina yao na
maafisa watendaji wa Mitaa kwani kufanya kazi kwa Ushirikiano na Upendo
ndio silaha pekee ya kuimarisha utendaji na ufanisi wa ukusanyaji wa
mapato katika Mitaa.
MD
Kayombo ameyasema hayo Wakati wa kikao cha kazi pamoja na wenyeviti wa
Mitaa kilichokuwa na dhamira ya kushauriana namna bora ya kuimarisha
mapato ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ili kuwa na uchumi imara,
kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa hiyo Mtaa wa Kibamba CCM
na kuhudhuriwa pia na Wakuu wa Idara na Vitengo.
Mkurugenzi
huyo amesema kuwa atazuru kata hadi Kata ili kubaini wapi kumwepwaya na
kipi kipaombele katika maeneo husika ili kuanza nayo katika kuimarisha
maendeleo ya wananchi.
Hata
hivyo wenyeviti wote wamekabidhiwa Bendera, Rejista, Vitini vyenye
miongozo ya kisheria sambamba na vitini vinavyobainisha majukumu ya
Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ili kutoingiliana katika utendaji na
viongozi wengine wakiwemo watendaji wa Mitaa na Kata.
Naye
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob ambaye pia ndiye
alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho amesema kuwa wenyeviti wanapaswa
kuwasimamia vyema wananchi kulipa kodi kwani hiyo ndiyo njia pekee ya
Manispaa kujisimamia yenyewe na kujiendesha kirahisi.
Mstahiki
Meya ametumia Kikao hicho kumpongeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndg
John Lipesi Kayombo kwa uongozi wake imara na uliothubutu kwani
umewafanya wananchi katika Manispaa hiyo kuwa walipaji wazuri wa kodi.
Jacob
amesema kuwa mipango ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ni kuifanya
Manispaa hiyo kuwa ya mfano na kuzishinda Manispaa zingine katika Jiji
la Dar es salaam.
Kuhusu
Posho za wenyeviti wa Mitaa, Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo amewasihi
wenyeviti kuwa na subira kwani wanaandaa mpango imara kwa kushirikiana
na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ili kuwalipa malimbikizo ya posho zao
zote wanazodai.
Pia
amewasihi wenyeviti hao kutumia Uhuru wao kikatiba kuwafungulia kesi
wale wote wanaowaonea, kuwazalilisha na kuwakejeli kwa kuwafungulia kesi
katika mahakama kwa mujibu wa sheria.
SHARE
No comments:
Post a Comment