Mgodi
wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu uliopo katika halmashauri ya Msalala
wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga umekabidhi hundi zenye thamani ya
zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya malipo ya ushuru wa huduma
kwa halmashauri ya Msalala iliyopo mkoani Shinyanga na halmashauri ya
wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita.
Hafla
fupi ya kukabidhi hundi hizo imefanyika Alhamis Machi 2,2017,katika
ukumbi wa halmashauri ya Msalala wilayani Kahama na kuhudhuriwa na
viongozi wa halmashauri na mikoa ya Shinyanga na Geita pamoja na
viongozi mbalimbali kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo,Meneja
mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Graham Crew alisema fedha hizo
ni malipo ya ushuru wa huduma kwa ajili ya kipindi cha miezi sita
kuanzia mwezi Julai hadi Disemba 2016.
Alisema fedha hizo ni asilimia 0.3 ya
ukokotoaji wa ushuru wa huduma ya mgodi huo kwa kipindi cha miezi sita
katika awamu ya pili kuanzia mwezi Julai hadi Disemba 2016.
“Mgodi umelipa shilingi za
kitanzania 1,135,178,526/= na malipo hayo yamegawanyika katika
halmashauri mbili kwa mujibu wa makubaliano na serikali ambapo
halmashauri ya Msalala imelipwa shilingi milioni 760 sawa na asilimia 67
na Nyang’wale shilingi milioni 374 sawa na asilimia 33”,alisema Crew.
Aidha alisema mpaka sasa mgodi huo
umelipa jumla ya shilingi bilioni 4.3 tangu mwaka 2014 kampuni ya Acacia
ilipoanza kutoa malipo ya ushuru wa huduma wa asilimia 0.3 ya mapato
ghafi kwa halmashauri husika.
“Katika kipindi cha miaka hiyo minne
halmashauri ya Msalala imelipwa zaidi ya shilingi bilioni 3.7 na
Nyang’wale imelipwa shilingi bilioni 1.1”,aliongeza Crew.
Katika hatua nyingine Crew alisema
mgodi huo unaendelea kushirikiana na serikali na wadau wa maendeleo ili
kutekeleza miradi mbalimbali kwa ajili ya kuboresha huduma endelevu za
kijamii na miundombinu katika jamii hususani katika
elimu,barabara,umeme,maji na huduma za afya.
Wakipokea hundi hizo,mkuu wa mkoa wa
Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga na Katibu tawala wa mkoa wa
Shinyanga Albert Msovela waliushukuru mgodi huo kwa kutimiza wajibu wa
kulipa kodi na kuongeza kuwa fedha hizo zitatumika katika shughuli za
maendeleo ya wananchi katika halmashauri za Msalala na Nyang’wale.
Mwandishi wetu,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa hafla hiyo,ametuletea picha za matukio yaliyojiri,tazama hapa chini
Wa pili kutoka kulia ni Mtaalamu wa
Mawasiliano Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu Mary Lupamba
akiwakaribisha viongozi wa mkoa wa Shinyanga na Geita wakati wa hafla
fupi ya kukabidhi hundi zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja
kwa ajili ya malipo ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya Msalala na
Nyang’wale.Wa kwanza kushoto ni Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu
Graham Crew,akifuatiwa na mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu
Ezekiel Kyunga na Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela
Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu
Graham Crew akiangalia hundi ya shilingi milioni 374 kabla ya kuikabidhi
kwa mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga kwa
ajili ya halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale .Kushoto ni Kiongozi wa
Kitengo cha Mahusiano ya Jamii mgodi wa Bulyanhulu Sarah Ezra Teri
Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu
Graham Crew akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 374 kwa
mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga kwa ajili ya
malipo ya ushuru wa huduma ya mgodi kwa halmashauri ya Nyang’hwale
iliyopo mkoani Geita
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu Graham Crew akishikana mkono na mkuu wa mkoa wa Geita Meja
Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga wakati akikabidhi hundi ya shilingi
milioni 374
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu Graham Crew akizungumza wakati wa kukabidhi hundi zenye
thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya malipo ya ushuru
wa huduma kwa halmashauri ya Msalala iliyopo mkoani Shinyanga na
halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita. Alisema halmashauri ya
Msalala imelipwa shilingi milioni 760, Nyang’wale shilingi milioni 374
Mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali
Mstaafu Ezekiel Kyunga akikabidhi hundi hiyo ya shilingi milioni 374 kwa
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale Carlos Gwamagobe
Mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali
Mstaafu Ezekiel Kyunga akizungumza wakati wa zoezi la makabidhiano ya
hundi yenye thamani ya shilingi milioni 374 kwa ajili ya halmashauri ya
wilaya ya Nyang’wale ambapo alisema fedha hizo zitatumika katika
shughuli za maendeleo ya wananchi katika halmashauri hiyo
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya
Nyang’wale Carlos Gwamagobe (kulia) akishikana mkono na Mkuu wa mkoa wa
Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga wakati wa makabidhiano ya
hundi hiyo
Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale Hamim
Gwiyama akishikana mkono na Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu Graham Crew wakati wa makabidhiano ya hundi ya shilingi
milioni 374
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu Graham Crew (kushoto) akizungumza wakati wa kukabidhi hundi
yenye thamani ya shilingi milioni 760 kwa ajili ya malipo ya ushuru wa
huduma ya mgodi kwa halmashauri ya Msalala iliyopo mkoani Shinyanga.
Katikati ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akifuatiwa
na mbunge wa jimbo la Msalala Ezekiel
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu Graham Crew akishikana mkono na katibu tawala wa mkoa wa
Shinyanga Albert Msovela wakati wa kukabidhi hundi ya shilingi milioni
760 kwa ajili ya halmashauri ya wilaya ya Msalala iliyopo wilayani
Kahama mkoani Shinyanga
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu Graham Crew akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hiyo ambapo
alisema halmashauri ya Msalala imelipwa shilingi milioni 760 sawa na
asilimia 67
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu Graham Crew akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ya hundi
ya shilingi milioni 760
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu Graham Crew akishikana mkono na mbunge wa jimbo la Msalala
wilayani Kahama Ezekiel Maige
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga
Albert Msovela akizungumza wakati wa kupokea hundi yenye thamani ya
shilingi milioni 760 ambapo alisema aliushukuru mgodi huo wa malipo ya
ushuru na kuongeza kuwa tayari fedha hizo zimeshaingizwa kwenye bajeti
ya halmashauri ya Msalala kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri hiyo.
Meneja mkuu wa mgodi wa dhahabu wa
Bulyanhulu Graham Crew akishikana mkono na Mweka hazina halmashauri ya
Msalala Masatu Mnyolo aliyemwakilisha mkurugenzi wa halmashauri ya
Msalala wakati wa kukabidhi hundi hiyo
Mbunge wa jimbo la Msalala Ezekiel
Maige akizungumza wakati wa makabidhiano hayo ambapo aliuomba mgodi huo
kuendelea kulipa kodi kama inavyostahili huku akiomba mgodi kuyabana
makampuni yanayofanya kazi zake mgodini ili yalipe kodi kwa ajili ya
maendeleo ya halmashauri ya Msalala
Meneja Mkuu wa Mahusiano ya Kampuni ya
Uchimbaji ya Acacia na Serikali Mhandisi Asa Mwaipopo akizungumza wakati
wa makabidhiano hayo ambapo alisema Acacia imetimiza wajibu wa kulipa
ushuru na kufanya tukio la kukabidhi hundi hizo kwa uwazi zaidi ili
kuepuka minong’ono kuwa pengine mgodi huwa haulipi kodi
Meneja Mkuu wa Mahusiano ya Kampuni ya
Uchimbaji ya Acacia na Serikali Mhandisi Asa Mwaipopo alisema kodi
iliyolipwa imetokana na uzalishaji wa mgodi kwa kipindi cha miezi sita
na hiyo ni awamu ya pili,utaratibu wa Acacia ni kulipa kwa miezi 6 na
tayari awamu ya kwanza walishalipa na sasa wamemalizia kipindi cha pili
katika mwaka 2016
Meneja Mkuu wa Mahusiano ya Kampuni ya
Uchimbaji ya Acacia na Serikali Mhandisi Asa Mwaipopo alisema kampuni ya
Acacia imekuwa ikifanya kazi zake kwa kushirikiana na wananchi
wanaozunguka migodi yao
![](https://4.bp.blogspot.com/-8Noao8ATsAA/WLiHSzvZDMI/AAAAAAAANVg/VR2G5yV9i1sh0fI8cRVOQv-qkT2vH02UQCEw/s640/a.jpg)
Meneja Mkuu wa Mahusiano ya Kampuni ya
Uchimbaji ya Acacia na Serikali Mhandisi Asa Mwaipopo akishikana mkono
na mbunge wa jimbo la Msalala Ezekiel Maige
![](https://1.bp.blogspot.com/-YlsRkZ0yIsI/WLiHUQsOJCI/AAAAAAAANVg/EZBy05iK4Ew1cKMaw0fp4MvUVcJkWhD0QCEw/s640/b.jpg)
Meneja Mkuu wa Mahusiano ya Kampuni ya
Uchimbaji ya Acacia na Serikali Mhandisi Asa Mwaipopo akiagana na katibu
tawala mkoa wa Shinyanga Albert Msovela.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
SHARE
No comments:
Post a Comment