Mradi
wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi Kupitia Tasnia ya urembo ujulikanao
kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation
wataendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Mbeya
kuanzia Jumatatu, tarehe 8 March 2017 kwenye ukumbi wa SIDO Mkoani
Mbeya. Mafunzo hayo yatatolewa kwa jumla ya wanawake watakaochaguliwa 30
kutoka mkoani Mbeya.
Baada
ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa Taasisi
hiyo kwa lengo la kuhakikisha wanawake wa Mkoa wa Mbeya wanafikia
malengo yao waliojiwekea katika kujikita kwenye kujiajiri. Wanawake
wakazi wa Mkoa wa Mbeya waliotuma maombi kupitia tovuti ya Manjano
Foundation na wanaopenda kunufaika na mradi huo wanaombwa kujitokeza kwa
ajili ya usaili siku ya Jumatatu tarehe 6 Machi 2017 kuanzia saa tatu
(9:00AM) asubuhi kwenye ukumbi wa wa SIDO Mkoani Mbeya.
Mafunzo
yana lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea
kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya
kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa
biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha na
pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake.
Awamu
ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi
sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. Baada yanawake hawa kuhitimu
mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation itawaunganisha na taasisi za
fedha zinazotoa mikopo bila riba waweze kupata mtaji wa kununua bidhaa
za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa chini ya
uangalizi maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.
Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 658 741711 au +255 712 378516
SHARE
No comments:
Post a Comment