Mama Salma Kikwete
aliwaongoza wazazi kumpokea mwanae Rashid Jakaya Kikwete na watoto wengine kwenye
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, waliporejea nyumbani kutoka
Marekani walikotwaa medali za dhahabu katika mashidnano ya uwezo kitaaluma ya Genius Olympion ambayo yalishirikisha
jumla ya nchi 63 Dubiani. Wanafunzi hao kutoka shule ya sekondari ya wavulana, Feza
Boys ya Kawe jijini Dar es Salaam, ni pamoja na Rashidi Jakaya Kikwete, mtoto wa
Rais mstaafu Jakaya Kikwete, Abdulrazak Juma Nkamia, Mtoto wa Mtangazaji wa zamani
wa redio, ambaye sasa ni Mbunge wa Chemba Mkoani Singida, Juma Nkamia, na
Abdallah Rubeya.
Mama Salma aliwapongeza
wanafunzi hao kwa kufanya vizuri katika mashindano hayo lakini pia kwa
kuitangaza Tanzania.
SHARE
No comments:
Post a Comment