Rais
Dkt John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake ,Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn aliyewasili hivi punde katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam.
Waziri
Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn akipewa maua ikiwa ni ishara ya
kumkaribisha kwa upendo nchini Tanzania,mara baada kuwasili katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
mapema leo mchana,na baadae kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt John
Pombe Magufuli,Waziri Mkuu Kassim Majliwa na viongozi mbalimbali wa
Kitaifa.
Waziri
Mkuu wa Ethiopia ,Hailemariam Dessalegn akishuka kwenye ndege mara
baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere mapema
leo mchana,na baadae kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe
Magufuli,Waziri Mkuu Kassim Majliwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa.
Imeelezwa kuwa ujio wa Waziri huyo Mkuu wa Ethiopia ni pamoja
na kukuza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na Ethiopia
pamoja na kujadili fursa zaidi za ushirikiano katika maeneo mbalimbali
ikiwemo uwekezaji na biashara.
Mhe.
Dessalegn atakutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli kwa mazungumzo na kushuhudia uwekwaji saini
wa mikataba ya ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali kabla ya kuzungumza
na Waandishi wa Habari.
SHARE
No comments:
Post a Comment