Na Mwandishi wetu,
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imedhamiria kuanzisha
mtandao mpana wa majadiliano na wadau mbalimbali, zikiwemo Wizara
zinazohusika na Kilimo na Taasisi mbali mbali za Serikali na Binafsi,
ili kukubaliana vipaumbele na namna ya kushirikiana katika kufanikisha
utekelezaji wa majukumu ya TADB.
Hayo yamebainishwa na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga wakati akichangia mada
wakati wa Kongamano la Tatu (3) la Sera kuhusu Kilimo linaloendelea
katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.
Bw. Assenga alisema kuwa kwa kushirikiana
na wadau mbali mbali wa maendeleo kutachagiza kusaidia uwekezaji mkubwa
kwenye Sekta ya Kilimo, na kuleta mapinduzi ya kilimo nchini.
Alitolea mfano wa juu ya
umuhimu wa ushirikiano na wadau mbali mbali kwa kutaja utekelezaji wa
vitendo wa Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Morocco kwa kuingi
Mkataba na Benki ya Kilimo ya Morocco (yaani Kundi la Utoaji wa Mikopo
kwenye Kilimo nchini Morocco) ambayo yamelenga katika maeneo mbali mbali
yahusuyo maendeleo ya kilimo, hususan upatikanaji wa fedha.
Kwa upande wa mikopo, Bw. Assenga, TADB imekuwa
ikitoa mikopo ya muda mfupi; muda wa kati; na muda mrefu kwa Wakulima
wadogo wadogo, wa kati na wakubwa, hususan kuziba pengo la upatikanaji
wa fedha kwenye minyororo ya thamani katika sekta za kilimo, mifugo,
uvuvi na mazao ya misitu (ufugaji nyuki).
Bw. Assenga amesema kuwa
mpaka sasa Benki imekopesha jumla ya shilingi 6.5 Bilioni kwa kukopesha
vikundi 20 vyenye jumla ya wakulima 2575.
“Vile vile Benki imeweza
kuvijengea uwezo vikundi 336 vya wakulima wadogowadogo vyenye jumla wa
wanachama 44,400 katika mikoa ya Iringa, Morogoro na Tanga. Hivyo
kuwezesha jumla ya vikundi 19 kutimiza masharti na maandalizi ya msingi
ya kuweza kukopa; Vikundi vingine vilivyobaki vinaendelea kupatiwa
mafunzo ili viweze kufikia hali ya kuweza kukopesheka,” aliongeza Bw.
Assenga.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Kulia) na Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa Kuendeleza Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT – CTF), Dkt. John Kyaruzi (Kushoto) wakifuatilia mada wakati wa Kongamano la Tatu (3) la Sera kuhusu Kilimo katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.
Wadau walioshiriki Kongamano la Tatu (3) la Sera kuhusu Kilimo wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikiwasilishwa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Kulia) akichangia mada wakati wa Kongamano la Tatu (3) la Sera kuhusu Kilimo katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa Kuendeleza Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT – CTF), Dkt. John Kyaruzi.
Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa Kuendeleza Kilimo Kusini mwa Tanzania (SAGCOT – CTF), Dkt. John Kyaruzi (Kulia) akichangia mada wakati wa Kongamano la Tatu (3) la Sera kuhusu Kilimo katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam. Kushoto ni Bw. Alex Mkindi.
Wadau wakichangia hoja mbalimbali wakati wa Kongamano la Tatu (3) la Sera kuhusu Kilimo katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.
Mwezeshaji wa wa Kongamano la Tatu (3) la Sera kuhusu Kilimo, Prof. Andrew Temu (Aliyesimama) akizungumza na wadau waliojitokeza wakati wa Kongamano hilo.
SHARE
No comments:
Post a Comment