TRA

TRA

Monday, April 10, 2017

Mlipuko wa bomu Somalia waua watu 13

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Mkuu mpya wa jeshi la Somalia aliponea shambulizi la bomu la kujitoa mhanga hapo jana, muda mfupi tu baada ya kuapishwa na kupewa jukumu la kuanzisha operesheni mpya dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali. Watu 13 waliuawa katika shambulizi hilo.

Jenerali Mohamed Ahmed Jimale alikuwa ameapishwa tu na akawa katika msafara wa maafisa wengine wakuu wa jeshi wakati bomu lilipuka karibu na majengo ya wizara ya ulinzi mjini Mogadishu.

                 Moja ya milipuko ya mabomu nchini Somalia

Wanajeshi watano na raia wanane waliokuwa kwenye basi dogo lililopita karibu waliuawa. Kundi la al-Shabaab lilidai kuhusika na shambulizi hilo. 

Rais Mohamed Abdullahi Mohamed wiki iliyopita aliitangaza Somalia kuwa eneo la kivita na kuwapa msamaha wanamgambo watakaojisalimisha ndani ya siku 60 na kujiunga na upande wa serikali. 

Rais Farmaajo kama anavyofahamika aliwafanyia mabadiliko viongozi wa jeshi na kumteua mkuu mpya wa polisi.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger