TRA

TRA

Monday, April 10, 2017

Maelfu waandamana Budapest kupinga sheria dhidi ya chuo kikuu

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Maelfu ya watu waliandamana jana katikati ya mji mkuu wa Hungary, Budapest kupinga sheria ambayo huenda ikakilazimu chuo kikuu kimoja kufunga milango yake nchini humo. 

Zaidi ya waandamanaji 70,000 walikusanyika nje ya jengo la bunge, wakimtaka Rais Janos Ader kuipinga sheria hiyo, iliyopitishwa bungeni wiki hii na chama cha siasa mrengo wa kulia Fidesz cha Waziri Mkuu Viktor Orban.

Baadhi ya waandamanaji
Chuo Kikuu cha Ulaya, kilichoasisiwa na mfadhili wa Kimarekani George Soros, kwa sasa kina zaidi ya wanafunzi 1,400 kutoka zaidi ya nchi 100 na kinaendeshwa kwa mfumo wa kidemokrasia wa "jamii ya wazi", na kwenda kinyume na mipango ya Waziri Mkuu Orban ya kuwa na taifa linalopinga sera za kiliberali. 


Sheria hiyo itakihitaji chuo hicho kubadili jina lake na kufungua tawi lake Marekani na pia kuwako na makubaliano ya kisheria kuhusu chuo hicho kati ya Hungary na Marekani.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger