Rais Recep Tayyip Erdogan (pichani), ameonya kuwa jitihada za Uturuki
zinazokabiliwa na changamoto za kujiunga na Umoja wa Ulaya zitaendelea
kujadiliwa baada ya kura ya maoni ya wiki ijayo, inayolenga kumuongezea
madaraka, hali inayoibua mashaka kuhusu mustakabali wa mpango wa nchi
hiyo kupata uwanachama.
Katika hotuba yake aliyotoa akiwa mjini Izmir,
katika pwani ya Aegean, Erdogan alitishia kwa mara nyingine baada ya
kura hiyo ya maoni ya Aprili 16 kuidhinisha kuwa sheria kurejeshwa kwa
adhabu ya kifo -- kama itapitishwa bungeni -- hatua ambayo itamaliza
moja kwa moja jitihada zake za kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya.
Alisema Waturuki wanaoishi Ulaya wanaonewa na kudhalilishwa. Jana
ilikuwa siku ya mwisho ya upigaji kura kwa Waturuki wanaoishi ng'ambo.
Karibu nusu ya wapiga kura milioni tatu waliosajiliwa katika mataifa ya
kigeni, wanaishi Ujerumani.
SHARE









No comments:
Post a Comment