Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na wananchi mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori (Kulia), Diwani wa Kata ya
Kimara Mhe Manota wakikagua eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa
shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Kimara wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori wakati akizungumza nao mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota akizungumza na wananchi wa Kata hiyo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori kuzungumza na wananchi mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akiwaongoza wananchi kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akikagua ukarabati wa
Zahanati ya Mavurunza mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule
ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
ambapo ameahidi kusaidia kukamilika haraka kwa ujenzi huo.
Hali ya ukarabati wa Zahanati ya Mavurunza iliyopo katika Mtaa wa Mavurunza Kata ya KImara
Diwani
wa Kata ya Kimara Mhe Manota akimuongoza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe
Kisare Matiku Makori kukagua ukarabati wa Zahanati ya Mavurunza mara
baada ya kuzuru kukagua eneo hilo. Leo Mei 26, 2017 ambapo ameahidi kusaidia kukamilika haraka kwa ujenzi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na wananchi mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Mavurunza Kata
ya Kimara Jijini Dar es salaam muda mchache kabla ya kumkaribisha Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo kuzungumza na wananchi wa Kata hiyo. Leo Mei 26,
2017
Wananchi wa Kata ya Kimara wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori mara baada ya kuzuru kujionea eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata hiyo Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Baadhi ya Wakazi wa Kata ya Kimara wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori wakati akizungumza nao mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na wananchi mara baada ya kuzuru kukagua eneo litakalojengwa Shule ya Sekondari ya Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam. Leo Mei 26, 2017
Na Mathias Canal, Dar es salaam
Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori Leo Mei 26, 2017 ameiagiza
Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo inayoongozwa na Ndg John
Lipesi Kayombo kuanza haraka ujenzi wa Shule ya Sekondari kwa ajili ya
Kata ya Kimara Jijini Dar es salaam.
Agizo
hilo amelitoa wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi
Mvurunza mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Kata hiyo ili
kujionea hali ya maendeleo ya elimu sambamba na kubaini changamoto
zinazowakabili wananchi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ubungo na
hatimaye kuzitatua.
Katika
ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo imehudhuriwa pia na Katibu
Tawala wa Wilaya ya Ubungo, Afisa Tarafa ya Kibamba, Afisa Elimu
Sekondari Manispaa ya Ubungo, Diwani wa Kata ya Kimara, Mtendaji Kata ya
Kimara, Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa sambamba na Baadhi ya Wananchi
wa eneo hilo.
Agizo
la Mkuu wa Wilaya ya Ubungo linakuja zikiwa ni siku chache zimepita
tangu kutoa maagizo kama hayo katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza, Shule
ya Msingi Kawawa na Shule ya Sekondari Mburahati ambapo kote huko
ameelekeza kuanza haraka ujenzi wa Madarasa sambamba na Vyoo kwa ajili
ya wanafunzi na walimu.
Mhe
Makori alisema kuwa madarasa anayoagiza yaanze kujengwa yatapunguza
kadhia ya mbanano wa wanafunzi darasani ambapo pia amewaahidi wananchi
hao kujengwa madarasa kwa viwango vya kisasa.
Naye
Moses Mzakwe na Deogratius Stephano ambao ni wakazi wa Mtaa wa
Mavurunza wameomuomba Mkuu wa Wilaya kutilia mkazo swala la upimaji wa
viwanja ili wananchi waweze kumiliki ardhi huku wakimpongeza kwa kuzuru
katika eneo hilo kwani ameonyesha uwezo wa kujali wananchi anaowaongoza.
Awali
akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya kuzungumza na wananchi
hao Diwani wa Kata ya Kimara Mhe Manota alimpongeza Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kwa
kutekeleza sera na kuisimamia ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015/2020 na
kuwaomba watanzania wote kwa kauli moja pasina itikadi za vyama kumuunga
mkono kwani atakuwa imara na madhubuti zaidi katika utendaji wake iwapo
ataungwa mkono na watanzania wote.
Alisema
kuwa Rais Magufuli anapaswa kutilia mkazo zaidi kwa kuwawekea kufuli
watu waliokuwa wanalihujumu Taifa kwa wizi na ufisadi katika sekta
mbalimbali nchini.
Mhe
Manota alisema kuwa tayari zimetolewa jumla ya shilingi milioni mia
moja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Shule hiyo ambapo mara baada ya
kukamilika itawarahisishia wanafunzi kupata elimu bora pasina mateso
wanayoyapata sasa kutokana na ukosefu wa shule ya serikali ya Sekondari
katika Kata nzima ya Kimara.
SHARE
No comments:
Post a Comment