Kampuni ya Jumia Travel imeanzisha kampeni iliyopewa jina la 'Democratize Travel',ya kuwakomboa waafrika kusafiri ndani na nje ya mipaka yao kwa ghrama nafuu kupitia mtandao wa kampuni hiyo .
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Mkazi wa Jumia Travel nchini, Fatema Dharsee amesema bara la Afrika limekuwa katika mabadiliko ya matumizi ya Mtandao na kufanya kuongezeka kwa mapato ndani katika sekta ya Utalii.
Amesema kampeni hiyo ina dhumuni la kuondoa mawazo yaliyojengeka miongoni linapokuja suala la mchakato mzima wa kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine pamoja kupunguzwa kwa gharama za malazi.
Fatema amesema idadi ya watumiaji wa internet imezidi kuongezeka kwa bara la Afrika na kufikia watumiaji milioni 300 sawa na asilimia 27.7. Matumizi ya Internet yameweza kuchochea ukuaji wa shughuli za utalii kwa njia ya mtandao ikiwemo na usafiri wa anga.
Fatema amesema kutokana na takwimu hizo zinafanya kuamini Bara la Afrika lina fursa katika ukuaji wa sekta ya Utalii kwa njia ya mtandao.
Amesema ripoti ya utalii Afrika 2017 iliyowasilishwa na Jumia Travel inajihusisha na huduma za hoteli kwa njia ya mtandao , ambapo inaonyesha kuwa huduma za simu zimeiingizia Bara la Afrika mapato ya ndani kwa asilimia 6.7 kwa mwaka 2015 sawa na dola za Kimarekani bilioni 150 na itaongezeka kufikia dola za Kimarekani bilioni 210 sawa na asilimia 7.6 ya jumla ya pato la ndani la kitaifa kufikia 2020.
"Jumia Travel nimeona ujio wa Internet na kupokelewa vizuri na waafrika ni ishara kwamba sekta ya utalii itakua ukizingatia ina mchango mkubwa kwenye kuchangia pato la Taifa",alisema Fatema.
Meneja Mkazi wa Jumia Travel nchini, Fatema Dharsee akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari,wakati wa uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina la 'Democratize Travel',ya kuwakomboa waafrika kusafiri ndani na nje ya mipaka yao kwa ghrama nafuu kupitia mtandao wa kampuni hiyo,kushoto ni Meneja Uhusiano wa Umma,Godfrey Kijanga .
Meneja Uhusiano wa Umma-Jumia Travel ,Godfrey Kijanga akitoa ufafanuzi kuhusiana na kampeni hiyo 'Democratize Travel' inavyoweza kurahisisha mambo mbalimbali kwa wateja wao,ikiwemo suala la kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine,kulia ni Meneja Mkazi wa Jumia Travel nchini, Fatema Dharsee
Mwakilishi kutoka hoteli ya Hong Kong ya jijini Dar Es Salaam,Dusa Suleiman akielezea namna Jumia Travel inavyoweza kurahisisha ufanyikaji wa shughuli za kila siku za hoteli,amebainisha kuwa wao wamenufaika kwa kiasi kikubwa kuliko hapo awali kupitia mtandao huo wa Jumia Travel,amesema kupitia mtandao huo wateja wameweza kujua huduma zao mbalimbali,hivyo wateja wao wameongezeka .
Baadhi ya Waandishi wa habari wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa na Meneja Mkazi wa Jumia Travel nchini, Fatema Dharsee kuhusiana na uzinduzi wa kampeni iliyopewa jina la 'Democratize Travel',ya kuwakomboa waafrika kusafiri ndani na nje ya mipaka yao kwa ghrama nafuu kupitia mtandao wa kampuni .Picha na Michuzi JR.
SHARE
No comments:
Post a Comment