Staa wa filamu ‘grade one,’ ‘Jacqueline Wolper’.
Staa
wa filamu ‘grade one,Jacqueline Wolper’ ametokwa povu si la nchi hii
baada ya kubanwa kuhusiana na madai ya kunuka mwili na kusema hajawahi
kunuka maishani mwake na kwamba ingekuwa hivyo asingepapatikiwa na
wanaume. Hivi
karibuni Ijumaa lilimfungia kazi msanii huyo nyumbani kwake na katika
moja ya maswali aliyobanwa lilikuwa juu ya ishu iliyosambaa kuwa eti
anatoa harufu mbaya sehemu za mwili wake.
Katika
kuonesha kumaindi ile mbaya kuhusu madaia hayo, mrembo huyo ambaye
kiukweli yuko bomba kwa muonekano alifunguka: “Aliyekuambia nanuka nani?
Mimi sinuki wala sijawahi kunuka maishani mwangu, kuthibitisha hilo
kwanza nisingekuwa napapatikiwa na wanaume kila kukicha sambamba na
kuhongwa vitu kibao huku wengine nikiwaacha wakinililia.
Hao
wanaosema na kusambaza hayo ni njia tu ya kujipatia followers kwenye
mitandao yao kupitia mimi.” Wolper hakuishia hapo aliendelea kumwaga
povu kuwa, tangu afungue duka la nguo ambalo amewekeza zaidi ya shilingi
milioni 60, watu wengi wamekuwa wakichukizwa na maendeleo hayo. “Wana
chuki tu na mimi, tangu nimefungua duka wananichokonoa, wanalishadadia
hili jambo kisa tu nimepata mafanikio ya kufungua duka,” alipigilia
msumari.
SHARE
No comments:
Post a Comment