Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe.
Uhuru Kenyatta wakati wa ibada Maalum ya kuliombea Taifa la Kenya
iliyoandaliwa na Bunge la nchi hiyo. Wengine katika pichani kutoka
kushoto ni Spika wa Bunge la Kenya Justin Muturi, Spika wa Bunge la
Seneti la Kenya Mhe Ekwee Ethuro na Jaji Mkuu wa Kenya Jaji David
Maraga. Mhe Ndugai yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa mwaliko
Bunge la Kenya ambapo amembatana na wajumbe wa Tume ya Utumishi ya
Bunge, Mhe Mary Chatanda, Mhe Salim Turky na Mhe Mch.Peter Msigwa.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai (katikati ya waliokaa kulia)
akizungumza na Rais wa Kenya Mhe Uhuru Kenyatta na Makamu wake Mhe
William Rutto walipokutana wakati wa ibada Maalum ya kuliombea Taifa
hilo. Wengine katika picha ni Spika wa Bunge la Kenya Mhe Justin Muturi
(kulia kwa Mhe Ndugai),Spika wa Bunge la Seneti la Kenya Mhe. Ekwee
Ethuro (wa kwanza kulia),Mke wa Rais wa Kenya Margaret Kenyatta na Mke
wa Makamu wa Rais wa Kenya Rachel Chebet.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania (wa pili kulia) Mhe Job Ndugai akizungumza na Spika
wa Bunge la Seneti la Kenya Mhe Ekwee Ethuro (wa pili kushoto). Mhe
Ndugai yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa mwaliko Bunge la
Kenya ambapo amembatana na wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge, Mhe
Mary Chatanda, Mhe Salim Turky na Mhe Mch.Peter Msigwa.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akizungumza na Spika wa Bunge la
Seneti la Kenya Mhe Ekwee Ethuro alipomtembelea Ofisini kwake Jijini
Nairobi, Kenya. Mhe Ndugai yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa
mwaliko Bunge la nchi hiyo.
(Picha na Ofisi ya Bunge)
SHARE
No comments:
Post a Comment