Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na askari katika jaribio la kupora fedha.
Watu walioshuhudia tukio hilo lililotokea jana Jumapili wamesema mtu
huyo akiwa na wenzake walijaribu kupora fedha kwenye gari kabla ya
kuwekwa kwenye mashine ya kielektroniki ya kutolea fedha (ATM) ya benki
moja iliyopo katika jengo la makao makuu ya Idara ya Uhamiaji, Kurasini
jijini Dar.
“Aliyekufa aliamriwa asipite barabara hii, alipokataa kusimama polisi
walipiga risasi hewani, naye alipotaka kutoa bastola ndipo polisi
walipomfyatulia risasi na alikufa papo hapo,” amesema shuhuda wa tukio
hilo na kuongeza kuwa
wengine waliokuwa na mtu huyo walikimbia na mmoja amekamatwa.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema atazungumzia tukio hilo leo
SHARE
No comments:
Post a Comment