TRA

TRA

Monday, May 15, 2017

WENYE SUKARI MBEYA WAUNDA CHAMA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Muuguzi mkuu Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, Thomas Isdory akitoa hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi wa Hospitali hiyo wakati wa uzinduzi wa Chama cha WenyeKisukari Tawi la Rufaa
Dk. Jamil Kajuna ambaye ni mtaalam wa magonjwa ya Kisukari kwa Watoto akielezea dalili za ugonjwa wa kisukari wakati wa uzinduzi wa Chama cha Wenye Kisukari Tawi Tawi la Rufaa Mbeya.
Mkuu wa Idara ya tiba ya Kisukari katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, Dk.Sangare Antony akielezea umuhimu wa Wagonjwa wa kisukari kuwa na Chama ili kubadilishana mawazo.
Mtaalam wa Chakula na Lishe katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, Joyce Komba akielezea tiba ya sukari kwa wagonjwa ni kuzingatia ulaji wa vyakula kwa mpangilio.
Baadhi ya wagonjwa wa kisukari wakipata ushauri na vipimo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.



WAGONJWA wa Kisukari nchini wametakiwa kuzingatia ushauri wa Wataalamu kuhusu ulaji wa vyakula vya lishe na ufanyaji wa mazoezi hali itakayopelekea kupona kabisa kwa ugonjwa huo.
Rai hiyo ilitolewa juzi na Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, Thomas Isdory alipomwakilisha Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Dk. Godlove Mbwanji wakati wa ufunguzi wa Chama cha Wenye kisukari Tawi la Hospitali.
Alisema Wagonjwa wa kisukari wanapaswa kuzingatia ushauri wa Wataalamu kwani wao wanatakiwa kupewa elimu zaidi namna ya ulaji wa vyakula ili kuweza kumuda na kufahamu jinsi ya kuifanya sukari iliyopo mwilini kuwa katika kiwango stahili bila kuleta madhara
Alisema kupitia Chama cha Wenye kisukari itachangia wanachama wenyewe kwa wenyewe kutembeleana na kupeana elimu kuhusu ugonjwa wa kisukari na namna ya kukabiliana nao.
Aliongeza kuwa Hospitali ya Rufaa inajitahidi kuendelea kuboresha huduma kila siku ili wateja wao ambao ni wagonjwa waweze kupata matibabu yanayotakiwa na kwakati husika ikiwemo upatikanaji wa Dawa na vifaa tiba.
Awali Mkuu wa Idara ya Tiba ya Kisukari katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya, Dk. Sangare Antony alisema Wizara ya Afya iliagiza kila wenye magonjwa ya kudumu kuunda vyama vyao wakiwemo wenye kisukari jambo lililofanyika sasa.
Alisema lengo la kuunda chama cha wenyekisukari ni kuweza kujadili namna ya kukabiliana na changamoto mbali mbali wanazokumbana nazo katika kupata matibabu pamoja na kutambuana wenyewe kwa wenyewe.
Naye kiongozi wa Chama hicho Tawi la Hospitali ya Rufaa, Jane Simkoko katika Risala yao kwa mgeni rasmi alisema hadi sasa kinawanachama 224 kutoka Wilaya za Mikoa ya Mbeya,Njombe, Iringa na Rukwa ambao wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya.
Alisema chama hicho kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa vifaa, elimu kuhusu dalili za ugonjwa wa sukari,kukosekana kwa huduma vijijini, kukosekana kwa elimu juu ya mtindo bora wa maisha, kushindwa kuwafuatilia wagonjwa wasiopata tiba pamoja na ukosefu wa fedha za kuendeshea chama.
Aliongeza kuwa tayari wanachama 157 wamepatiwa kadi za uanachama ambapo pia Kampuni ya Philips imeweza kuwapa vifaa vya kupimia sukari kwa gharama nafuu.
Hata hivyo Dk. Jamil Kajuna na Joyce Komba waliwaeleza wanachama hao dalili za ugonjwa wa Sukari namna ya kupata matibabu pamoja na vyakula na aina ya milo ambayo mgonjwa anatakiwa kutumia ili kuweza kukabiliana na kupanda ama kushuka kwa sukari mwilini.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger