Miss Tanzania namba mbili 2006 na
Kaimu Katibu Hamasa wa Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha
Mapinduzi (UVCCM), Jokate Mwegelo akikabidhi zawadi mbalimbali kwa
wanafunzi wa Kidato cha Sita wa shule ya Sekondari ya Jangwani mara
baada ya kumaliza mtihani wao.
Miss Tanzania namba mbili 2006 na
Kaimu Katibu Hamasa wa Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha
Mapinduzi (UVCCM), Jokate Mwegelo akikabidhi cheti kwa wanafunzi wa
Kidato cha Sita wa shule ya Sekondari ya Jangwani mara baada ya kumaliza
mtihani wao.
Kaimu Mkuu wa shule ya Jangwani, Amos Mgongolwa akizungumza katika mahafali hayo
Jokate Mwegelo akizungumza katika mahafali hayo
Dada Mkuu wa shule ya Jangwani akimrisha keki Jokate katika mahafali hayo
………………………………
Na Mwandishi wetu
Mwanamitindo, muigizaji na Miss
Tanzania namba mbili 2006, Jokate Mwegelo ametoa wito kwa watu maarufu
nchini kusaidia kuondoa changamotokatika sekta mbalimbali ili kupunguza
mzigo serikali.
Jokate alisema hayo wakati wa
mahafali ya wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari ya
Jangwani ambapo jumla ya wanafunzi 118 walimaliza shule.
Mrembo huyo ambaye ni Kaimu Katibu
Hamasa wa Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)
amesema kuwa Tanzania ina watu wengi maarufu na wenye uwezo, lakini
wachache tu ndiyo wamekuwa wakijitolea kusaidia sekta mbalimbali
husasani elimu na afya.
Alisema kuwa kwa hali
ilivyosasa,ni vigumu kwa serikali kutatua matatizo yote na kuwaomba
wanamuziki, wasanii, wafanyabiashara na viongozi mbalimbali wa vyama na
serikali kujitolea kusaidia kutatua matatizo katika jamii.
Alifafanua kuwa shule ya wasichana
ya Jangwani ni kongwe kutokana na kuanzishwa Mei 28, 1928, lakini
mpaka sasa inakabiliwa na matatizo mbalimbali wakati kuna wahitimu wengi
ambao kwa sasa wana nyandhifa na wanashindwa kuchangia.
“Mimi sijasoma Jangwani, lakini
niliguswa na matatizo ya viwanja vya michezo na kuamua kujenga uwanja wa
mpira wa kikapu na mpira wa pete (netiboli), nashukuru viwanja kwa sasa
vinatumiwa na shule zinazozunguka maeneo haya,naomba wengine wasaidie,
kuondoa changamoto zilizopo,” alisema Jokate.
Mrembo huyo pia amewaomba viongozi
wa serikali na wafanyabiashara waliosoma katika shule ya Sekondari ya
wasichana ya Jangwani, kusaidia kuondoa changamoto za shule hiyo.
Awali, Makamu Mkuu wa Shule hiyo,
Amos Mgongolwa alisema mbali ya uchakavu wa majengo, shule yao haina
madarasa na mabweni ya kutosha, haina ukumbi wa kufanyia shughuli
mbalimbali kama sherehe na kulazimika kufanyia eneo la wazi, shule haina
hata gari moja kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwa pamoja na
matibabu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Mgongolwa amesema wanafunzi wenye
mahitaji maalum, ulazimika kutumia baiskeli za miguu mitatu ili kwenda
kwenye shughuli mbalimbali za kimamoso nje ya shule.
SHARE
No comments:
Post a Comment