Na Mwamvua Mwinyi, Kibiti
WAKATI
serikali ikijipanga kuanzisha Mkoa wa kipolisi katika wilaya ya Rufiji,
Kibiti ,Mafia na Mkuranga ,katibu wa CCM kata ya Bungu ,wilaya ya
Kibiti, Halife Mtulia amepigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Kibiti, Zena Mgaya, alisema
marehemu ameuawa majira ya saa 4 usiku may 13 .Alisema alipata taarifa
la tukio kutoka kwa viongozi wa CCM kata. Zena alieleza Mtulia ameuawa
akiwa anatoka uwani mwa
nyumba yake kwenda kuoga akiwa ameshika ndoo ya maji ndipo wauaji
wawili walipojitokeza na kumuua kisha kutokomea kusikojulikana. Wauaji
hao walitumia usafiri wa pikipiki kwa kuiacha mbali na eneo la tukio na
baada ya kutimiza adhma yao walitembea kuifuata walipoipaki kisha
kuondoka “alielezea Zena.Alisema Marehemu alikuwa Katibu wa CCM Kata ya
Bungu, Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa kutoka wilaya ya Kibiti na
mjumbe wa Serikali ya kijiji Nyambunda na ameacha mke na watoto. Zena
alisema kufuatia matukio ya mauaji kijiji cha Nyambunda kata ya Bungu
kimeshapoteza Mwenyekiti wa kiiji, Mtendaji wa Kijiji, na wenyeviti
watatu wa vitongoji vilivyoko katika kijiji hicho .Alipoulizwa kuhusiana
na uchaguzi wa ndani ya chama unavyoendelea ngazi ya shina na matawi
Zena alisema wanachama wanagomea kujitokeza.Uchaguzi wa safari hii ni
mgumu hakuna anaejitokeza kugombea kabisa, watu wanahofu “alifafanua.Nae
Asha Hemed na Ramadhani Swedy walisema hali bado ni mbaya kiusalama
katika wilaya hiyo na Rufiji.
Walisema jeshi la polisi lisambaze askari wake na maeneo ya vijijini ambako wahalifu hao ndio wamejikita huko.
Matukio hayo ni pamoja na Jan 19,ambapo mjumbe wa serikali ya kijiji cha Nyambunda ,Oswald Mrope, aliuawa kwa kupigwa risasi.
March 1,mwenyekiti wa kijiji cha Nyambunda Said Mbwana aliuawa.
Octoba
24,2016 afisa mtendaji wa kijiji cha Nyambunda Ally Milandu alipigwa
risasi na kufa na novemba 6,2016 .Tukio jingine ni lile la mwenyekiti wa
kitongoji cha Nyang’unda kijiji cha Nyambunda Mohammed Thabiti alipigwa
risasi akielekea kwake.
Jeshi
la polisi Pwani limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai ,
linaendelea kupambana na kuwasaka wahalifu na kuimarisha ulinzi.
SHARE
No comments:
Post a Comment