TRA

TRA

Thursday, May 25, 2017

Kiongozi wa upinzani azuiwa kuingia Zambia

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Polisi nchini Zambia wamemzuia kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Afrika kusini kuingia nchini Humo.

Mmusi Maimane kutoka chama cha Democratic Alliance, alikuwa akitarajiwa kuhudhuria kesi inayomkabili kiongozi wa upinzani nchini humo Haikande Hichilema.

 Kiongozi wa Upinzani nchini Afrika kusini Mmusi Maimane

Bwana Hichilema anashtakiwa kwa makosa ya uhaini baada ya kushindwa kutoa njia kwa msafara wa Rais wa Zambia, hali ambayo inadaiwa kuhatarisha maisha ya mkuu huyo wa nchi.

Kiongozi huyo wa upinzani nchini Afrika kusini Mmusi Maimane amesema amelazimika kurudi nyumbani baada ya maafisa kuingia ndani ya ndege ya Shirika la ndege la Afrika kusini aliyokuwa amesafiri nayo mjini Lusaka, kumvamia na kumnyang'anya simu yake.

Hata hivyo bado hakuna taarifa zozote zilizotolewa na serikali ya Zambia.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger