Klabu ya Uingereza ya Everton itazuru nchini Tanzania kwa mechi za kirafiki kabla ya msimu wa 2017/18.
Everton itakuwa klabu ya kwanza ya ligi ya Uingereza kucheza katika taifa hilo la Afrika Mashariki, na itakabiliana dhidi ya mshindi wa kombe hilo la Sportpesa.
- Simba sasa yadhaminiwa na SportPesa
- SportPesa watoa udhamini kwa Serengeti Boys
- Kenya kucheza dhidi ya Hull City Uingereza
Mapema mwezi huu Everton ilitangaza udhamini wa mamilioni ya pesa na Sportpesa ambapo jina la kampuni hiyo ya kamare litakuwa mbele ya tisheti za mabingwa hao wa Uingereza kwa miaka mitano.
Tangu kuanzishwa kwake nchini Kenya 2014 kampuni hiyo imedhamini vilabu vingi, kuwekeza mbali na kushiriki katika kamari.
SHARE
No comments:
Post a Comment