TRA

TRA

Monday, May 15, 2017

LG YAZINDUA BIDHAA YA MPYA YA KIYOYOZI INAYOTUMIA UMEME MDOGO NA RAFIKI KWA MAZINGIRA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

 Mkurugenzi Mtendaji LG Electronics Afrika Logistics, Janghoon Chung akingumza na waandishi habari juu ya ubora wa viyoyozi vya LG iliyofanyika jana  katika Hoteli ya Hyatt Legency jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi wa Masoko Afrika Mashariki LG Electronics , Moses Marji  akizungumza wakati wa  uzinduzi wa bidhaa mpya kutoka LG Meneja wa bidhaa za LG Afrika Mhandisi , Singh Chana  akizungumza juu ya umuhimu wa bidhaa za LG katika uhifadhi wa Mazingira. Mkurugenzi Mtendaji LG Electronics Afrika Logistics, Janghoon Chung Akimkabidhi zawadi ya Televisheni mmoja wa washindi wa bahati nasibu, Bw. Rama Esteem, iliyochezeshwa katika semina ya uzinduzi wa bidhaa mpya za Lg Tanzania.


 Viyoyozi vinavyotunza mazingira

KUTOKANA na kuongezeka kwa mahitaji ya matumizi ya

viyoyozi vinavyotunza mazingira na matumizi madogo ya

umeme Afrika Mashariki na Kati, LG Electronics Afrika

Mashariki na Kati kwa kushirikiana na Kampuni ya EVAC

ambayo ni msambazaji wa ndani, walikutana na wadau wa

viwanda kujadili matokeo na fursa kwa njia ya matumizi

inayofaa.

Semina kuhusu suala hilo ilihudhuriwa na zaidi ya washiriki

100, wakiwemo washauri wa miradi wakubwa, wakandarasi,

wasanifu majengo na wabunifu wa ndani wa majengo kuunda

Tanzania ya baadaye yenye teknolijia rafiki kwa mazingira.

Katika tukio hilo, LG kama mvumbuzi wa teknolojia ya

viyoyozi rafiki kwa mazingira, walionyesha uwezo wao mkubwa

kwa kutumia teknologia ta Inverter, ambayo yameundwa

kutunza upozaji kwa muda mrefu Afrika mashariki na kati na

ambapo inachangia kuelekea mazingira ya kijani.

Akiongea katika tukio hilo, Janghoon Chung, Mkurugenzi

Mtendaji wa LG Electronics Africa Logistics FZE alisema:

"Eneo la Afrika Mashariki na kati limeanza kuwa na uelewa

mkubwa wa umuhimu wa kutumia bidhaa rafiki kwa mazingira

endelevu . Na kwa muendelezo wa miji safi na mipango miji ya

Mashariki ya kati na Afrika, Hali ya hewa ya Joto, Bidhaa za

kupasha joto, viingiza hewa na Viyoyozi (HVAC) na vifaa vya

sokoni vimelenga kuleta matumizi makubwa katika makazi

tofauti ya watu,sehemu za biashara na viwanda. Makampuni

yanawekeza katika R&D na ubunifu wa bidhaa mpya ambazo

zina nguvu na zinatumia garama ndogo za matumizi ya nishati,"

alisema.

 Pamoja pia na mwitikio kutoka kwa wadau wa viwanda

ikiwemo LG Bidhaa za kuongeza joto, upozaji na viyoyozi

(Heating, Ventilation and Air Conditioning(HVAC)  sekta ya

viwanda inatarajia ongezeko kubwa miaka ijayo kutokana na

kuongezeka kwa mahitaji”. Tunajivunia kuzindua njia hizi za

matumizi leo hapa Tanzania na tunauhakika zitatengeneza

biashara imara na mabadiliko chanya katika jamii.”

"LG inatambua kwamba linapokuja swala la viyoyozi, wateja

katika eneo husika sasa wanatafuta zaidi ya kiyoyozi chenye

uwezo wa Kuleta ubaridi. Kwa kuongezea kukamilisha udhibiti

wa hali joto, Mfumo wetu mpya wa viyoyozi unaleta faida za

matumizi na matumizi madogo ya nishati. Kwa kutumia

teknolojia ya “Quiet Inverter” na usafishaji wa hewa safi na

salama (high quality air purification and sterilization systems)

Mtumiaji anaweza kufurahia mazingira salama kwa afya yake

aliongeza Janghoon Chung.

Viyoyozi vya LG vimebuniwa katika maumbo mazuri na

teknolojia bora iliyobuniwa kuwa njia mahususi kwa miezi ya

Joto. Mfumo wa bidhaa bora za Multi V VRF umeongeza

mahitaji ya wadau muhimu kama wakandarasi,washauri na

wajenzi  kwa sababu ya ufanisi wake , majibu ya haraka ya

kiufundi na huduma baada ya mauzo. Utafiti wa upande wa

tatu wa soko umethibitisha kuwa bidhaa za LG zinaongoza

katika ukanda huu.

Kasi kubwa ya ukuaji wa haraka wa teknolojia katika uzalishaji

wa HVAC, njia za matumizi za kisasa zimeundwa na tabia

ambazo zinaleta matumizi mazuri ya nishati na rafiki kwa

mazingira, kwa kushirikiana na vigezo vya serikali na mahitaji

ya wateja. Bidhaa zinazoendana na teknolojia ya kijani zinapata

uungwaji mkono mkubwa kutokana na sheria za matumizi ya

nishati kitaifa na kimataifa.

Kwa kufuata sheria za HVAC zinazotumika katika ukanda

kama  kupata vibali vya LEED (Leadership in Energy &

Environmental Design) certification, Africa Energy Efficiency

Building Regulations, and GCC Standardization Council

(GSO), kati ya vingine, LG Electronics inahakikisha bidhaa

kwa uangalifu zinatimiza vigezo vya matumizi ya nishati

vilivyowekwa na mamlaka za udhibiti , serikali na

watengenezaji wengine wa  sera  za mipango miji katika nchi

husika katika ukanda .

Biashara ya HVAC za LG imekua kwa kasi ndani ya miaka 20

iliyopita. Mafanikio ya viyoyozi vya LG yamekuwa mpaka

kufikia kuwa moja ya wazalishaji wakubwa katika ushindani wa

HVAC . Biashara ya Viyoyozi vya LG tayari ni sehemu

muhimu ya biashara ya kampuni na LG imewekeza katika

kuzalisha njia za matumizi bora katika makazi ya watu na sekta

za biashara kwa miongo mingi sasa.

LG Electronics, Inc. (KSE: 066570.KS) ni mvumbuzi

anayeongoza kimataifa katika teknolojia katika vifaa

vinavyotumia umeme ,simu za mkononi na vifaa vya

nyumbani, imeajiri watu 75,000 wanaofanya kazi katika vituo

118 vya kazi duniani kote . Ikiwemo mauzo ya kimataifa ya

2016.ya dola za kimarekani  47.9 bilion   (KRW 55.4 trillion),

LG inaendesha michepuo minne ya biashara ? Vifaa vya

nyumbani & udhibiti hewa , mawasiliano, Burudani za

nyumbani na vifaa vya magari ? na ni moja ya wazalishaji

wanaoongoza wa Luninga bapa, simu za mkononi ,viyoyozi,

mashine za kufulia na majokofu. Kwa habari zaidi na taarifa

kuhusu bidhaa za LG , tafadhali tembelea

www.LGnewsroom.com.

Kuhusu kampuni ya bidhaa za umeme za mfumo wa hewa ya

LG

Kampuni ya bidhaa za umeme za mfumo wa hewa ya LG

inaongoza kimataifa katika uzalishaji wa vifaa vya ndani

viyoyozi na mfumo bora wa udhibiti hewa.

Kampuni inatengeneza mfumo kamilifu wa nyumbani   kwa

viwanda vyake kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu. LG

imedhamilia kuboresha maisha ya wateja duniani kote kwa

kuzalisha bidhaa zilizobuniwa kisasa, ikiwemo

majokofu,mashine za kufulia ,mashine za kuoshea vyombo

,majiko ya umeme, Vivuta vumbi ( vacuum cleaners), Vifaa ya

kujengea ndani (built-in appliances), Viyoyozi, vishafisha hewa

(, air purifiers) na vifaa vya kupunguza unyevunyevu (

dehumidifiers). Kwa ujumla , bidhaa hizi zinaleta ufanisi wa

hali ya juu, Mtumizi bora , huduma nzuri na faida za kiafya

.Kwa maelezo zaidi , tafadhali tembelea  www.LG.com.












Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger