TRA

TRA

Thursday, May 25, 2017

Man United kusajili nyota wapya watatu au wanne

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Antoine Griezmann moja kati ya nyota wanaowindwa na Man United

Mabingwa wa taji la Europa ligi msimu huu klabu ya Manchester United inatarajiwa kuweka kikomo cha kufanya usajili kwa wachezaji watatu au wanne muhimu katika dirisha kubwa la usajili.

Meneja wa United Jose Mourinho amesema makamu mwenyekiti wa timu hiyo Ed Woodward anajua wachezaji wanaotakiwa kwa zaidi ya miezi miwili iliyopita.

"Ed Woodward anayolisti yangu ya wachezaji ninaowataka ," alisema meneja huyo baada ya mchezo wa Europa ligi dhidi ya Ajax .

Mourinho anataka kuongeza changamoto katika safu ya ulinzi na ushambuliaji ili kuweza kuwania taji la ligi kuu ya England msimu ujao. 

United wamekua wakihushwa na kutaka kuimarisha safu ya ushambuliaji kwa kuwasajili Antoine Griezmann toka Atletico Madrid, Andrea Belotti wa Torino pamoja Romelu Lukaku. 

Kwa Upande wa safu ya ulinzi wachezaji wanaotajwa kuwa wako kwenye rada ya Mourinho ni beki wao wa zamani Michael Keane anayechezea Burnley,beki kisiki wa Benfica Victor Lindelof na Muholanzi Virgil van. Dijk wa Southampton.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger