Mbunge
wa Arusha Mjini Mh. Goodbless Lema amemshukuru Mbunge Lazaro Nyalandu
kwa kufanikisha safari ya Marekani ya watoto watatu ambao walinusurika
kifo katika ajali ya basi la shule ya Lucky Vicent iliyotokea Karatu na
kusababisha vifo vya watu 35.Mh. Nyalandu alikuwa bega kwa bega na
kufuatilia kila hatua kuhakikisha watoto hao pamoja na wazazi wao na
daktari wanasafiri kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kupata matibabu
zaidi. Mh
Lazaro Nyalando , Mungu akubariki sana kwa kazi nzuri ya kusaidia
watoto waliopatwa na ajali hapa Arusha, jitihada zako Mungu atakulipa"
alisema Godbless Lema Katika hatua nyingine Mh Lazalo Nyalandu ameomba
pesa zitakazo endelea kuchangwa na Watanzania na watu wengine duniani
kwa ajili ya watoto hao zitumike kujenga ICU katika hospitali ya Mount
Meru.
"Kwa
kuwa wadau wanaendelea kuchangia na kwa kuwa shule ya sekondari
zimekubali kuanzisha mfuko ambao wanausimamia wenyewe na kwa kuwa mfuko
huo lengo lao kubwa lilikuwa kuwasafirisha hawa watoto kazi ambayo
imefanywa na Samaritan Purse lakini lengo la pili ilikuwa ni kwenda
kuwatibu kazi ambayo inafanywa na Shirika la STEMM kwa kushirikiana na
Hospitali kuu ya Mercy hivyo kazi itakayobaki Mh Mkuu wa Mkoa itakuwa
ndogo, kwa hiyo nimeomba na nimeshaurina nao na wamekubali kwamba
Watanzania na wanadunia wote watakao endelea kuchanga fedha zote ziletwe
kwako Mh Mkuu wa mkoa ili ziweze kujenga kituo cha wagonjwa ambao
wanahitaji huduma ya haraka (ICU) katika hospitali yetu ya Mount Meru"
alisema Nyalandu
SHARE
No comments:
Post a Comment