Mdau mkubwa wa klabu ya Simba, Mohammed
Dewji ‘MO’ ameiandikia klabu hiyo barua (demand note) ya kuitaka kumlipa
fedha zote za mishahara alizokuwa akiwalipa wachezaji tangu mwaka jana
kiasi cha shilingi bilioni 1.4 baada ya kubaini kuwa klabu hiyo imeingia
mkataba na kampuni ya SportPesa bila kumshirikisha.
Hayo yamejiri siku moja baada ya Simba
kutiliana saini mkataba wa udhamini na kampuni ya SportPesa. Uongozi wa
Simba ukiongozwa na Rais wa timu, Evans Aveva, ulisaini mkataba huo wa
miaka mitano na kampuni ya SportPesa wenye thamani ya Sh. 4.9 bilioni.
MO amewaandikia Simba ‘demand note’ kwa
kuwa wamekiuka makubaliano yao kwamba, atoe fedha kama makubaliaono ya
kuingia kwenye mfumo wa hisa na ikitokea kampuni inataka kuidhamini
Simba inabidi wakae meza moja viongozi na MO ili hiyo kampuni itambue
mwelekeo wa Simba, lakini viongozi wa klabu hiyo wakasaini kimyakimya.
Klabu hiyo ya Simba imeanza mchakato wa
marekebisho ya katiba yao ili kuruhusu kipengele cha uwekezaji kwa mfumo
wa hisa kama lilivyokua ombi la MO kuwekeza katika klabu hiyo kwa
asilimia 51 za hisa huku wanachama wakibaki na asilimia 49.
SHARE
No comments:
Post a Comment