Maelfu wamekusanyika Berlin kumsikiliza rais wa zamani
wa Marekani Barck Obama na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani wakijadili
demokrasia na wajibu wa dunia katika Siku ya Kanisa.
"Kwanza kabisa nafikiri siku hii ya Kanisa mwaka huu kwa vyoyote vile
ni tukio maalum sana kwa sababu sio siku zote tunasheherekea miaka 500
ya mageuzi.Huu ni mwaka maalum sana wa kumkumbu ya Martin Luther jambo
ambalo linaturudisha kwenye historia."Kansela Angela Merkel wa Ujerumanianetanka hayo wakati akizungumza wakati ameketi pembezoni mwa Obama mbele ya hadhira ya tukio hilo alipongezwa na Obama kwa kufanya kazi ya kupigiwa mfano akiwa kama kiongozi wa taifa ambapo pia alisema ana furaha kurudi tena katika mji wa Berlin ambao anaupenda.
Obama amesema yuko furahani kurudi Berlin na sio tu kwamba anaupenda mji huo bali kutokana na kwamba mmojawapo wa washirika wake vipenzi katika muda wote alipokuwa rais alikuwa ameketi pembezoni mwake leo hii.
Azungumzia urithi wake
Katika maadhimisho hayo rais huyo wa zamani wa Marekani Barack Obama alizungumzia urithi au haiba aliyoiacha nyuma na maadili ya kiliberali ambayo ameyapigania akishirikiana na Kansela Angela Merkel.
Rais huyo wa zamani pia ameyatafakari mafanikio yake na yale mambo ambayo ameshindwa kuyafanikisha akiwa rais ambapo moja ambalo amesema linalomtia wasi wasi "hawakuweza kuzifanya huduma za afya zipatikane kwa kila mtu katika nchi yake" na maendeleo yalioyofanikshwa na utawala wake sasa yako hatarini.
Pia ametafakaari kushindwa kwake kukomesha vita vya Syria ambapo amesema ni vita katili na licha ya juhudi zao hawakuwa na zana zinazostahiki wakati wote kuweza kuleta mabadiliko katika eneo hilo.
Obama amesema "Matumaini yangu ni kwamba hivi sasa wakati sio tena rais lakini bado nina matumaini ya kuwa na ushawishi kidogo kwamba nitakuwa katika nafasi ya kusaidia vijana wengi zaidi kukabiliana na baadhi ya changamoto,kukishajiisha kizazi kipya cha uongozi ili kwamba tuweze kuwatenga wale wanaojaribu kutugawa na kuwaleta pamoja watu wengi zaidi wanaojaribu kutuunganisha kwa maslahi ya pamoja.Na nafikiri h´hapa ni mahala pazuri pa kuanzia."
Siku ya Kanisa ni jukwaa la majadiliano mazito,jukwaa kwa mdahalo wa kisiasa juu ya masuala ya hivi sasa.Ni tukio kubwa kabisa ambalo hufanyika kila baada ya miaka miwili mapema wakati wa majira ya kiangazi ni tamasha la kumfurahisha kila mtu.Wengi wa washiriki wa matukio 2,500 yanayofanyika katika kipindi cha wiki moja kusherekea Siku ya Kanisa wanakuwa ni vijana wenye umri wa chini ya miaka 30.
SHARE
No comments:
Post a Comment